Jennifer
Livigha (Team Leader wa ChingaOne blog - kulia ) akiwa pamoja na
mtembeaji maeneo ya Sam Nujoma Road mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam akiwa njiani kuelekea Mikocheni kwenye studio za Clouds FM.
Tanzania ni nchi yangu,Taifa Star ni timu yangu, Amka.......Saa ya Uzalendo imefika..... maneno
haya yametumika kama kauli mbiu ya Mtembeaji ........ ni maneno yenye
kuleta hamasa kubwa kwenye masikio ya kila mzalendo, ni maneno yenye
kuonyesha ari, nguvu na kutia moyo kwa yoyote ambaye ni mzalendo. Ni
kijana mwenye nguvu na shughuli zake zinazoweza kumuingizia kipato na
kuweza kuishi....... lakini kutokana na uzalendo alionao kwa nchi yake
na mapenzi makubwa aliyonayo kwa timu yake ya Taifa aliamua kufanya
safari ndefu ya miguu kutoka Mbeya hadi jijini Dar es salaam akiwa na
nia ya kuja kuipa nguvu timu yake ya Taifa star. Watu wengi tunaamini
uzalendo huonekana pale mtu anapojiingiza kwenye siasa, ila hili
litabadili fikra za watu na kujua kuwa uzalendo upo sehemu nyingi
ikiwemo hii.....
Binafsi anasema safari
yake anaiita Uzalendo Tour na nia kubwa ni kuiunga mkono timu ya
Taifa Stars, anashukuru sana kwa nguvu aliyoipata toka alipoanza safari
yake , watu wengi wamejitokeza sehemu mbalimbali toka Mbeya hadi Dar es
salaam na kuweza kumpigia simu, kumpa vitu mbalimbali vilivyoweza
kufanya safari yake kuwa rahisi. Wazo lake lilikuwa la muda mrefu sana
lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake alishindwa
kulitekeleza kwa wakati huo. Safari ya miguu kwa kilometa nyingi kama
hizo sio rahisi kwa yoyote ila kutokana na Uzalendo wake ameweza
kutimiza ndoto yake, Safari yake amekuwa akiifanya muda wa mchana na
giza linapoingia alilazimika kupanda gari..... anamshukuru sana Gerald
Hando wa PowerBreakfast wa Clouds fm kwa moyo na nguvu kubwa aliyoitumia
katika kufanikisha safari hii.
...UZALENDO KWANZA..
Chanzo: Chingaone.com
No comments:
Post a Comment