HUDUMA YA UTOAJI WA TAARIFA ZA WAHAMIAJI HARAMU YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM
Watanzania
wametakiwa kuitumia vema huduma mpya ya utoaji taarifa za wahamiaji
haramu pamoja na taarifa za waathirika wa biashara hiyo, ili kupata
msaada na kupunguza kasi ya biashara hiyo nchini.
Huduma
hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam na shirika la kimatiafa la
Wahamiaji (IOM) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Haji Janabi ametoa wito wa
matumizi sahihi ya huduma hiyo katika kutoa taarifa za wahamiaji haramu
pamoja na vitendo vya biashara haramu ya binadamu.
Huduma
hiyo ambayo ni kitabu chenye namba za simu za vyombo mbalimbali,
vikiwemo vyombo vya dola vinavyotoa msaada wa haraka, imekuja wakati
ambapo Tanzania imekuwa ikishuhudia ongezeko la matukio ya wahamiaji
pamoja na biashara haramu ya binadamu.
No comments:
Post a Comment