Vijana wakiwa makini kufuatilia vipengele vya rasimu ya katiba mpya.
Kijana akichangia mawazo katika marekebisho ya rasimu ya katiba mpya.
Vijana wakiendelea kujadiliana jinsi ya kurekebisha rasimu ya katiba mpya.
Hawa ni baadhi ya vijana walifika katika ukumbi wa Mr. Price City uliopo mjini Moshi katika mchakato wa kuchangia mawazo katika rasimu ya katiba mpya.
MOSHI vijana wa manispaa ya Moshi wameendelea kutoa maoni yao kuhusu rasimu ya katiba mpya katika ukumbi wa Mr. Price City uliopo mkabala na ofisi kuu za Tanesco mjini Moshi. Leo ndio majumuisho yanafanyika na mapungufu makuu yaliyojitokeza katika rasimu ya sasa ni;
1. Raisi wa jamuhuri aamepewa madaraka makubwa na yupo juu ya sheria.
2. swala la kuwa na serikali tatu linapunguza utengamano wa muungano.
3. rasimu imetoa ufafanuzi wa kina kuhusu haki za mtoto lakini haijaeleza kijana ni nani, wajibu na haki zake?
4. rasimu haijaonesha makundi ya walemavu hayaja shirikishwa kwa kila mchakato.
5. rasimu haijaongelea lolote kuhusiana na uengamano wa Tanzania katika jumuia ya africa mashariki. Mkutano huu unaendelea leo ambapo makundi ya vijana walemavu wanapata nafasi yakutoa maoni yao.
Vijana wote mliopo katika manispaa ya Moshi mnakaribishwa katika ukumbi wa Mr. Price City leo kuanzia saa mbili na nusu asubuhi mpaka mchana saa sita.
******************************************************************************
No comments:
Post a Comment