Marehemu Said maarufu kama "Mwauwezo" akiwa amefunikwa na kanga na wasamaria wema muda mfupi baada ya ajali.
MOSHI Ajali
Mbaya iliyosababishwa na Gari aina ya Land cruiser ambayo Dereva wake
alikimbia Baada ya Kumgonga muendesha pikipiki (Bodaboda) Katika eneo la
Majengo Fire mjini Moshi Mkoani Kilimanajaro Usiku wa jana. Chanzo cha ajali hiyo hakikuweza kufahamika kwa haraka.
Ajali hiyo imepelekea kifo cha Dereva huyo wa pikipiki Aliyetambulika kwa Jina Moja la Said maarufu kama "Mauwezo" mkazi wa njoro mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, analiyesifika kwa Kuendesha Baiskeli kwa umahiri.
Baada ya Ajali hiyo polisi wa usalama barabarani walifika na kuchukua
vipimo ndipo kundi kubwa la waendesha bodaboda likajikusanya na kuanza
kuharibu gari lililosababisha ajali na mwishowe wakalichoma Moto
huku wakilia kwa sauti kubwa kitendo kolichopelekea Polisi wa Usalama
Barabarani kuondoka kwa kuhofu kujeruhiwa na vijana hao waliokua na
jazba.
#teamKINGJOFA
No comments:
Post a Comment