Mwenyekiti wa tamasha la Jambo Festival 2013,
Bw. Augustine Namfua.
Na.Mwandishi wetu.
ZAIDI
ya washiriki 100 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki kwenye
tamasha la Sanaa na utamaduni la Jambo Festival litakalofanyika oktoba
23 hadi 27 mwaka huu katika viwanja vya Suye vilivyopo mjini Arusha.
Mwenyekiti
wa tamasha hilo la Jambo Festival 2013 Bw. Augustine Namfua alisema kuwa
tamasha hilo ni la pili kufanyika mkoani Arusha ambapo wamekuwa
wakifanya kila mwaka lengo likiwa ni kuwawezesha washiriki mbalimbali
kuweza kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni kutoka ndani na nje ya nchi.
Alisema
kuwa tamasha hilo ambalo ni la kimataifa pia litawashirikisha
washiriki kutoka nchi za Ufaransa na Angentina ambao wataweza kuonyesha
matamasha mbalimbali ya kitamaduni sambamba na kuonyesha bidhaa zao za
kitamaduni.
Alisema
kuwa, tamasha hilo litaenda sambamba na matukio mbalimbali ya kiasili
ikiwemo maonyesho ya mavazi ya kiasili,pamoja na tamasha la kiasili
kutoka vikundi jijini Tanga, Arusha, na Dar es Saalamu.
Namfua
aliongeza kuwa, pia kutakuwepo na tamasha la muziki wa kisasa pamoja
na onyesho la mavazi , na ubunifu wa mavazi ambapo katika tamasha
hilo kwa siku hizo kila siku kutakuwa na matamasha mbalimbali ambayo
yatakuwa yakionyeshwa.
Aliongeza
kuwa, tamasha hilo limekamilika kwa asilimia 50 huku watu mbalimbali
wakiwemo binafsi, mashirika na taasisi mbalimbali zinazohusika na
maswala ya sanaa na tamaduni wanaendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili
ya kushiriki katika tamasha hilo.
"Tamasha
la mwaka jana lilifana sana kwani tuliweza kupata washiriki wengi sana
kutoka ndani na nje ya nchi na lilikuwa na mwitiko mkubwa sana , huku
watu mbalimbali wakipata fursa ya kuonyesha sanaa zao na tamaduni
mbalimbali na kuweza kujifunza kutoka kwa wenzetu wan je ya nchi ndio
maana tumeamua kufanya tena mwaka huu mwezi wa kumi hivyo tunatarajia
watu mbalimbali kushiriki kikamilifu katika tamasha hilo" alisema Namfua.
Aidha
aliwataka watu mbalimbali kufika katika tamasha hilo na kuonyesha
bidhaa zao za kitamaduni zinazotengenezwa kwa mikono pamoja na kutangaza
tamaduni zao za kiafrika , huku akiwataka wadau mbalimbali kuonyesha
moyo katika kusaidia matamasha hayo ili yaendelee kufanyika mara kwa
mara.
Credit: Mo Blog
No comments:
Post a Comment