MOSHI serikali wilayani Siha mkoani Kilimanjaro imetakiwa
kutoa maelezo yenye vielelezo vya kutosha kwa maandishi kuhusu ubovu wa jengo la ofisi ya mkuu wa
wilaya hiyo ambalo limemlazimu mkuu huyo kuhamia jengo jinguine la idara ya maji ilikupisha ukarabati.
Agizo hilo limetolewa na kamati ya
kudumu ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa wakati wa majumuisho ya
ukaguzi wa miradi ya maemdeleo wilayani hapo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Jonh
Iwanji amesema kamati hiyo imetoa siku
saba kwa serikali wilayani hapo kuwasilisha taarifa mbele ya kamati hiyo kwaajili ya kuchukuliwa hatua stahiki zaidi.
Naye mkuu wa wilaya ya hiyo Dr. Charles
Mlingwa amekiri kuhama katika jengo hilo baada ya wataalamu kutoka chuo kikuu
kupitia wakala wa ujenzi wa majengo ya
serikali nchini kumwagiza aondoke ili
kupisha ukarabati wa jengo hilo lililokuwa likihatarisha usalama wake.
Kwa upande wake
kaimu meneja wa wakala wa ujenzi wa majengo ya serikali mkoani Kilimanjaro Bw.
Audax Ngimbwi amesema mkandarasi wa jengo hilo ni JKT Suma na tayari hatua za awali zimechukuliwa ikiwa
ni pamoja na kuagizwa kulikarabati jengo
hilo.
No comments:
Post a Comment