Msemaji
toka Wizara ya Kazi na Ajira Bw.Ridhiwan Wema(Kulia) akieleza kwa
waandishi wa habari kuhusu majukumu ya Bodi za Mishahara Kisekta kwa
mujibu wa sheria Na. 7 ya Mwaka 2004 ya Taasisi za Kazi katika Sekta
Binafsi, wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) Leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mchumi Mwandamizi
wa Wizara hiyo Bw. Jofrey Mashafi.
Afisa
Kazi Mwandamizi toka Wizara ya Kazi na Ajira(kulia) akieleza kwa
waandishi wa habari(Hawapo pichani) jinsi ukuaji wa sekta unavyochangia
kuanzishwa kwa bodi ya Mshahara kwa Sekta husika wakati wa Mkutano
uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo jijini Dar es
Salaam. Msemaji Wizara hiyo Bw.Ridhiwan Wema.
Mchumi
Mwandamizi toka Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Jofrey Mashafi (kulia)
akieleza mipango ya serikali ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa
Ajira Nchini ikiwa ni pamoja kuanzisha programu ya miaka 3 inayoratibiwa
na Wizara ya Kazi na Ajira kwa kushirikiana Chuo cha Sokoine na Bank
ya CRDB ya kuwajengea uwezo wahitimu wa vyuo vikuu, inayotarajiwa
kuzalisha ajira 30,000, wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa
Idara ya Habari (MAELEZO) Leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa
Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Georgina Misama. (Picha na Frank
Mvungi-MAELEZO).
Credit: MoBlog
No comments:
Post a Comment