Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, November 12, 2013

KUZOROTA KWA MAENDELEO YA SHULE KUNACHANGIWA NA WAZAZI KUTOLIPA MICHANGO YA SHULE KWA WAKATI

SIHA imeelezwa kuwa baadhi ya wazazi kutokuchangia michango ya shule za msingi na sekondari kwa wakati  imekuwa ikichanguia kushuka kwa kiwango  cha elimu na kusababisha uendeshaji wa shule kuwa mgumu

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza ya Purming Godfrey Sauya wakati akizungumza na wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo katika maafali ya wanafunzi wa darasa la saba yaliyofanyika mwishoni mwa wiki

Alisema  baadhi ya wazazi wamekuwa wakichangia zaidi kushindwa kufikia malengo ya shule kutokana na kushindwa kulipa karo za wanafunzi kwa wakati jambo ambalo ni hatari katika kukuza elimu hapa nchini

Aliwataka wazazi wa wanafunzi wanasoma shule mbalimbali hapa nchni kuhahakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao wa kuwalipia wanafunzi wa michango ili waweze kupatiwa elimu bora kutokana  naa fedha watakazochangia ambazo zitaweza kununua vifaa  vya shule

Awali diwani wa Kata  ya Karansi Dancan Urassa alisema kuanzishwa kwa shule za msingi za watu binafsi zimechangia zaidi kupunza mlundikano wa wanafunzi  katika shule zinazomilikiwa na serikali jambo ambalo limechangia zaidi kupunga watoto wenye umri wa kwenda shule kukosa nafasi

Alisema jamii inatakiwa kuzitumia shule hizo kwani zimekuwa zikichangia zaidi katika kuboresha elimu na kuwataka wananchi kuacha  dhana ya kutochangia michango ya shule kwa madai kuwa shule hizo zipo chini ya wahisani
Nae mkaguzi wa shule wa Wilaya hiyo Robatha Assey   aliwataka wazazi na walezi   kupeleka watoto wao katika shule hiyo  ili waweze kupata elimu na kuwawezesha kujiendeleza kutokana na elimu inayotolewa shule hapo.

Awali akisoma taarifa ya kituo hicho, Mwanzilishi wa shule hiyo Mchungaji Wanaeli Mafie  alisema shule hiyo wenye wafadhili kutoka  kanisa la  Perimeta kutoka nchni Marekani ilianzishwa mwaka 2003 na tangu kuanzishwa imekuwa ikifaulisha kwa asilimia moja
 
Alifafanua kuwa katika matokeo  mtihani wa  darasa la saba mwaka huu shule hiyo imeshika nafasi ya pili  kati ya shule 52 kiwilaya na nafasi 30 kati ya 920 kimkoabaada ya kufaulisha wanafunzi wote walifanya mtihani huo.

No comments:

Post a Comment