Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, December 22, 2013

ADAIWA KUFARIKI DUNIA KWA KILE KINACHODAIWA NI ULEVI WA POMBE HARAMU AINA YA GONGO

MOSHI Leo asubui majira ya saa tano asubui mtu mmoja maarufu kwa jina la tall amekutwa akiwa amefariki kwenye nyumba maarufu kwa uuzaji wa pombe haramu aina ya gongo na bangi karibu na msikiti wa answari maeneo ya dar es salaam street mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Mashuhuda wa tukio hilo ambao ni wakazi na wafanyakazi wa eneo hilo kuona mwili wa kijana huyo waliita tax ili iweze kumpeleka hospital lakini dereva tax alipofika na kugundua kuwa kijana yule tayari ameshakata rogho alikataa kubeba mwili ule ndipo walipoamua kupiga simu polisi, na muda si mrefu polisi walifika eneo lile na kuweza kuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi.

   Lakini kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio lile walikuwa wakisikitika sana na kusema kwa mwaka huu tall ni mtu wa tatu kufariki katika nyumba ile, na waliendelea kusema kama vyombo husika wakilifumbia macho swala hili la watu kufanya biashara haramu na pia kusababisha vifo vya watu ni kwamba nguvu kazi ya taifa itazidi kupungua kadiri siku zinavyokwenda. Na chanzo makini cha mtandao huu wa Kingjofa Blog kilipojaribu kumtafuta mmiliki wa nyumba hiyo hakikufanikiwa kumpata ila jirani mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema "Mwenye nyumba amewaruhusu watu hao kuishi kwenye nyumba hiyo kama walinzi na hawalipi kodi ya nyumba na watu hao wameamua kugeuza nyumba hiyo kama danguro la pombe haramu na bangi".

Mtandao huu wa kingjofa Blog unaendelea kufuatilia taarifa kutoka katika jeshi la polisi na pia kufahamu nini hatima ya wakazi wa nyumba hiyo na pia kufahamu kama biashara hiyo ya pombe haramu na bangi itaendelea au itakomeshwa. Na pia kufahamu dhumuni la mwenye nyumba hiyo kuamua kuwaruhusu wakazi hao kugeuza nyumba yake kama sehemu ya kuuzia pombe haramu na bangi.

No comments:

Post a Comment