Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, March 3, 2014

HUU NDIO WARAKA WA SIRI WA CCM KUHUSU RASIMU YA PILI YA KATIBA..,

Huu ndio Waraka wa siri wa CCM kuhusu Rasimu ya Pili ya Katiba!

WARAKA NAMBA 3

 

CHAMA CHA MAPINDUZI

  

KIKAO CHA HALMASHAURI

KUU YA TAIFA

  

WARAKA KUTOKA IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA

 

TAARIFA KUHUSU RASIMU YA PILI YA KATIBA

Dodoma

Februari, 2014

UTANGULIZI
Mnamo tarehe 03/06/2013 Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitangaza Rasimu ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo kuwapa fursa wananchi kutoa maoni yao kupitia Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na Mabaraza ya Taasisi.
Kati ya mwezi Juni na Agosti 2013 Chama Cha Mapinduzi kilijiunda kama Baraza la Katiba la Kitaasisi kupitia mikutano ya wanachama na viongozi kuanzia ngazi ya matawi hadi taifa. Maoni ya mabaraza haya ndiyo yaliyokuwa msingi wa mapendekezo yaliyowasilishwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Tarehe 30/12/2013 Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitangaza Rasimu ya Pili ya Katiba ambayo itawasilishwa katika Bunge la Katiba ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kupata Katiba mpya.
Nia ya waraka huu ni kufanya uchambuzi utakaosaidia kupata uelewa wa pamoja wa Rasimu ya Pili na kutoa fursa ya kujipanga vizuri kwa hatua zinazofuata katika mchakato wa kuunda Katiba mpya. Kwa mantiki hii waraka huu unabainisha yafuatayo:
·         Maeneo  ambayo  mapendekezo   ya  CCM  yaliyotolewa  katika  Rasimu  ya Kwanza yamezingatiwa moja kwa moja;
·         Maeneo ambayo hayakuzingatiwa moja kwa moja, lakini yamezingatiwa kwa namna ambayo inakidhi mapendekezo yaliyotolewa na CCM;
·         Mambo mapya yaliyoingizwa kwenye Rasimu ya Pili;
·         Uchambuzi wa Rasimu na mapendekezo.         
Taarifa hii ina sehemu tatu. Sehemu ya Kwanza inaainisha jinsi  mapendekezo ya CCM yalivyopokelewa na Tume kama  ilivyotajwa  hapo  juu.  Sehemu  ya  Pili itabainisha changamoto za muundo unaopendekezwa (kisheria; gharama; kitaasisi, kwa mtazamo wa kujenga umoja wa taifa letu). Sehemu ya Tatu ina majumuisho na mapendekezo ya kurekebisha mfumo uliopo  kwa  kuzingatia  changamoto zilizotajwa na haja ya kuuimarisha Muungano.
SEHEMU YA KWANZA
MAPENDEKEZO YA CCM YALIVYOPOKELEWA NA TUME
1.      MAPENDEKEZO YALIYOZINGATIWA MOJA KWA MOJA
Ibara ya 9(3)
Ilipendekezwa ibara hii iondolewe kwa kuwa inazungumzia Serikali ya Muungano
kuweka Katiba kwenye mitaala ya elimu, ilhali elimu si mojawapo ya mambo ya
Muungano.
Pendekezo hili limezingatiwa kwa kuondoa ibara hii.
Ibara ya 22(3)
Ibara hii ambayo ilikuwa ibara ya 21(3) ya Rasimu ya Kwanza ilihusu kuweka
ukomo kwa wastaafu wanaopokea pensheni ya umma kushika nafasi za uenyekiti
au ukurugenzi katika mashirika ya umma.
CCM ilipendekeza  ibara hii irekebishwe ili wastaafu  waruhusiwe kuendelea
kutumia ujuzi wao katika nafasi watakazokuwa wamepewa kwa kuzingatia vigezo na uwezo wao wa kumudu majukumu hayo.
Pendekezo hili limezingatiwa na ibara hiyo ya 21(3) imeondolewa.
Ibara ya 26(2) 
Hii ilikuwa ibara ya 25(2)  katika Rasimu ya Kwanza. CCM ilipendekeza  ibara hii ifafanuliwe  ili  kubainisha  kuwa  ni  usafirishaji  haramu  wa  binadamu  ndiyo
unaopigwa  marufuku.
Pendekezo hili limezingatiwa kwa kueleza katika ibara ya 26(2) kuwa ni biashara haramu ya kusafirisha na kuuza binadamu.      
Ibara ya 32     
Hii likuwa Ibara ya 31ya Rasimu ya Kwanza.CCM ilipendekeza ibara hii iimarishwe
kwa kuandikwa upya ill itamke bayana kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano haina dini; Iakini watu wake wana uhuru wa kuabudu.
Pendekezo hili limezingatiwa kwa Ibara 1(1) ya Rasimu ya pili kutamka kuwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ni Shirikisho lisilofungamana na dini. Kadhalika,ibara ya 32(3) ya Rasimu inasema shughuli za uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya serikali.         ·
Ibara ya 47(1)
Hii  ilikuwa  ibara  ya  46(l)(d)  katika  Rasimu  ya  Kwanza  na  ilihusu  haki ya
mwanamke kupata ujira sawa na mwanaume. Ilipendekezwa  irekebishwe ili haki
hiyo ihusu kupata ujira sawa kwa kazi zenye sifa inayofanana.
2
Pendekezo hili limezingatiwa kwa Rasimu ya Pili kueleza katika ibara ya 47(1)(d) kuwa kila mwanamke ana haki ya  kupata fursa na ujira sawa na mwanaume katika kazi zenye sifa zinazofanana.       
Ibara y.a 79
Hii ilikuwa ibara ya 75 katika Rasimu ya Kwanza na ilihusu sifa za mtu anayetaka kugambea urais. CCM ilipendekeza wazazi wote wawili wawe raia wa kuzaliwa.
Pendekezo hili limezingatiwa kwa kueleza katika ibara ya 79(c) ya Rasimu ya Pili kuwa wazazi wote wawili wa mgombea wawe ni raia wa kuzaliwa.
Ibara ya 80
Hii ilikuwa ibara ya 77 katika Rasimu ya K anza. Ibara hii ilihusu kiwango cha ushindi kwa  mgombea  urais. CCM ilipendekeza  kwamba  mgombea  wa  urais atangazwe kuwa mshindi iwapo ntapata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote halali zilizopigwa.
Pendekezo limezingatiwa kwa_kueleza kuwa mshindi ni yule aliyepata asilimia hamsini ya kura halali zilizopigwa.
Ibara ya 83
Katika Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya 76 na ilihusu haki ya mtu kuchaguliwa kuwa Rais na ukomo wake. Ibara ndogo ya (4) ya ibara hii ilikuwa na mkanganyiko kuhusu uwezekano wa Makamu wa Rais aliyeko  madarakani kugombea urais endapo Rais ameshindwa kutekeleza. majukumu yake. Ibara hii haikueleweka vizuri kama Makamu huyu angeweza kuchaguliwa  kwa  kipindi kimoja tu au viwili kuwa Rais kwa kuzingatia muda ambao alikuwa akitumikia nafasi ya Makamu wa Rais. CCM ilipendekeza ibara hii ifafanuliwe vizuri kwani ilikuwa inakinzana na ibara nyingine zilizohusu nafasi ya Makamu wa Rais.       '
Pendekezo limezingatiwa ambapo Rasimu ya Pili katika ibara ya 83(4) imefafanua kuwa endapo Makamu wa Rais atashika nafasi ya madaraka ya Rais pale ambapo nafasi ya Rais iko wazi kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu, ataruhusiwa kugombea nafasi ya Urais kwa vipindi viwili, lakini kama atashika madaraka ya nafasi ya Rais kwa kipindi cha miaka mitatu au zaidi ataruhusiwa kugombea madaraka ya Rais kwa kipindi kimoja tu.                        
Ibara ya 90
Katika Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya 86(2) kuhusu Makamu wa Rais. Pendekezo la CCM lilihusu matumizi mazuri ya Kiswahili kwamba maneno Makamu atakuwa na jukumu la "kusababisha utekelezaji" yasomeke '"atawezesha au atasimamia utekelezaji".
Pendekezo limezingatiwa kwa kufafanua katika ibara ya 90(2) kuwa Makamu wa Rais atatekeleza au atasimamia utekelezaji wa jambo lolote...
3
Ibara ya 125
Katika  Rasimu  ya  Kwanza  hii  ilikuwa  ibara  ya  117(1)(a),  inahusu  sifa za
kuchaguliwa kuwa Mbunge. CCM il!pendekezwa umri uwe miaka 21 badala ya 25.
Pendekezo hili limezingatiwa katika ibara ya 125(1)(a) kuwa mgombea ubunge aliyefikisha umri wa miaka ishirini na moja anaweza kugombea ubunge.
Ibara ya 128
Katika Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya 123 na ilihusu mbunge kutopoteza ubunge wake iwapo atafukuzwa na Chama chake, isipokuwa kama  amejitoa mwenyewe. CCM ilipendekeza mbunge apoteze ubunge iwapo atafukuzwa au kwa hiari yake atajivua uanachama, na kwamba kigezo cha kupoteza ubunge kiwe ni uanachama na si namna mbunge alivyotoka kwenye chama chake.
Pendekezo limezingatiwa ambapo kwa mujibu wa ibara ya 128(1)(g) Mbunge atapoteza ubunge iwapo kwa ridhaa yake atajitoa au kujivua uanachama wa chama chake cha siasa, atafukuzwa au kuvuliwa uanachama wa chama chake cha siasa.
Ibaraya 133
Katika  Rasimu  ya  Kwanza  hii  ilikuwa  ibara  129 ycnye  maelezo  ya  pembeni
yaliyosomeka “ukomo wa mamlaka ya Bunge" huku maudhui yake yakihusu ukomo
wa Spika. CCM ilipendekeza maelezo ya pembeni (marginal notes) ya ibara hii yasomeke "ukomo wa mamlaka ya Spika". Ibara ya 129(1)(d) ilisema Spika atapoteza nafasi yake endapo atashindwa kuwasilisha "tamko rasmi" kwa Rais. CCM ilipendekeza utolewe ufafanuzi hili nitamko gani.
Mapendekczo ya kubadilisha maneno ya pembeni na ufafanuzi wa tamko rasmi yamczingatiwa ambapo imefafanuliwa katika ibara 133(1)(d) kuwa ni, tamko rasmi kuhusiana na mali na madeni yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Ibaraya 190
Katika Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya 181 iliyokuwa inaunda Tume Huru
ya Uchaguzi. Katika ibara ndogo ya (1) Rasimu iliipa Tume jukumu la kusimamia na kuratibu shughuli za vyama vya siasa. CCM ilipendekeza masuala haya yasiwe sehemu ya majukumu ya Tume.
Pendekezo limezingatiwa na jukumu la kuratibu na kusimamia shughuli za vyama vya siasa amepewa Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye ofisi yake sasa hivi inapendekezwa kuwa  taasisi huru.
Ibara ya 219  
Katika Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya 204, ilihusu kuondolewa madarakani
kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. CCM i!ipendekeza ibara ya 204 iboreshwe kwa kipengele kinachohusu  utaratibu wa kumwondoa
4
kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Ser:ikali kama ilivyo katika ibara ya 114(1)-(7)   ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka1977.
Pendekezo  limezingaliwa  ambapo  katika  ibara  ya  219  vimeongezwa  vipengele vinavyoelezea   namna na utaratibu ambao Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ataweza kuondolewa kazini pale itakapobidi.
Mpangilio wa namba za ibara
Katika Rasimu ya Kwanza kulikuwa na ibara ya 229 na ya 231. CCM ilipendekeza
mpangilio wa namba za ibara urekebishwe iii kuondoa kasoro ya kutokuwepo ibara       ya 230.
Pendekezo  limezingatiwa  kwa  namba  za  ibara  kurekebishwa  kwa  kuhakikisha mpangilio wa namba za ibara unafuata utaratibu.
Ibaraya 243
Katika Rasimu ya Kwanza  hii ilikuwa ibara ya 232, ambayo pamoja na ibara ya 227
zinahusu kuundwa  kwa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano,  ibara 232(1)
inaruhusu nchi washirika  kuunda vikosi vya Polisi. CCM ilip.endekeza_ibara  hii
iondolewe kwa nia ya kuepuka mgongano wa kiutendaji na kiusalama.
Pendekezo limezingatiwa ambapo kipengele cha 232(1) kinachohusu polisi wa nchi washirika kimeondolewa.
Ibara ya 248
Katika Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya 235 na ilihusu usalama wa Taifa
ambapo ibara.ya 235 ilihusu nchi washirika kuanzisha idara zao za usalama. CCM
ilipendekeza ibara hii iondolewe ili kuepuka  mgongano  wa  kiutendaji na wa kiusalama.
Pendekezo   limezingatiwa  ambapo  kipengele  cha  243(1)  kinachohusu kila nchi mshirika kuanzisha taasisi yake ya usalama wa Taifa kimeondolewa.
2. MAMBO   AMBAYO   YAMEZINGATIWA    KWA   NAMNA   INAYOKIDHI
MAPENDEKEZO YA CCM
Ibara ya 32
Hii ilikuwa ibara ya 31 iliyohusu uhuru wa imani ya dini. CCM ilipendekeza kwamba ibara hii iandikwe upya kwa kutamka bayana kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano haina dini lakini watu wake wana uhuru wa kuabudu.
Pendekezo hili  limezingatiwa katika  ibara 1(1) ya  Rasimu  ya  pili iliyotamka
Kuwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania  ni Shirikisho  lisilofungamana  na  dini.
Kadhalika ibara ya 32(3) ya Rasimu inasema shughuli za uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya serikali.
5

lbaraya56
Ibara hii inahusu uraia na katika Rasimu ya Kwanza maudhui yake yalikuwa katika
ibara za 54 hadi 56. CCM ilipendekeza kuweko uraia a nchi mbili.
Pendekezo hili limezingatiwa katika ibara ya 59 ya Rasimu ya Pili kwa kutoa
hadhi maalum  kwa watu walioacha  uraia  wa Tanzania  lakitti wana  asili au
nasaba ya Tanzania.
lbaraya 97
Maudhui  ya  ibara  hii  yamo  katika  ibara  ya  92 ya  Rasimu  ya  Kwanza CCM
ilipendekeza ibara ya 92(1) itaje kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri kama ilivyo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977.                                                                           
Pendekezo hili limezingatiwa kwa ibara ya 72(3)(a) na 97(2) kutaja kwamba Rais ataongoza mikutano ya Baraza la Mawaziri.
lbaraya125
Hii ilikuwa ibara ya 117 ya Rasimu ya Kwnnza. CCM ilipendekeza marekebisho ili mtu aliyetiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai asiwe na sifa ya kugombea Ubunge.
Pendekezo limezingatiwa ambapo kwa mujibu wa ibara ya (125)(2)(c) mtu aliyehukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita kwa kosa lolote anakosa sifa ya kugombea.ubunge.                                         
Ibara 137
Katika Rasimu ya Kwanza hii ilikuwa ibara ya 133 na ililmsu uteuzi wa Katibu wa
Bunge kufanywa na Tume ya Utumishi ya Bunge. CCM ilikuwa na maoni kwamba Tume ya Utumishi ya Bunge ndiyo ipendekeze majina matatu kwa Rais ambaye atafanya uteuzi wa jina moja la Katibu wa Bunge.
Pendekezo limezingatiwa katika ibara ya 137(1) ambapo Katibu wa Bunge atapatikana kwa Tume ya Utumishi wa umma kupendekeza majina matatu kwa Rais ambaye atateua jina moja.
3. MAMBO MAPYA
Kimsingi na kimaudhui Rasimu ya Pili haitofautiani sana na rasimu ya Kwanza. Rasimu ya Kwanza ilikuwa na sura 16 zenye ibara 239; Rasimu ya Pili ina sura 17 na ibara 271. Sura ya 17 haikuwepo, hivi sasa imeongezwa ili kubeba ibara zinazohusu masuala ya mpito.
Ibara ya 4(2)    '
Ibara hii inaelekeza kuwa lugha ya Kiingereza au lugha nyingine yoyote inaweza
kutumika kuwa lugha rasmi ya mawasiliano ya kiserikali pale itakapohitajika.
6
Ibara hii inaleta utaratibu mpya wa kurasimisha matumizl ya lugha mbalimbali katika mawasiliano ya kiserikali. Ikumbukwe kwamba hivi sasa upo utaratibu wa tafsiri kutolewa pale inapobidi kwa mfano mahakamani, kwa daktari na maeneo rnengine. Ingawaje ibara hii inapanua wigo wa mawasiliano ni vema ikachukuliwa kwa  tahadhari  ili isije ikafifisha  umoja  wa  kitaifa  uliojengwa  na  lugha  ya Kiswahili.
Ibara ya 49(1)(b)
Ibara hii inaeleza kuwa kila raia ana wajibu wa kulinda na kuheshimu Tunu za Taifa. Katika ibara ya 49(2) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajlli ya kuwawezesha raia kutekeleza masharti ya ibara hii.
Ibara inaainisha jambo la msingi kitaifa lakini si rahisi kuelewa ni katika mazingira gani raia anaweza akawajibishwa kisheria kulinda na kuheshimu tunu za Taifa.
Ibaraya 113
Kwa mujibu wa ibara hii Bunge la Muungano lifakuwa na Wabunge 50 toka Tanganyika, 20 toka Zanzibar na 5 kutoka kundi la watu wenye ulemavu watakaoteuliwa na Rais. Kila jimbo litatoa wabunge wawili mwanamke na mwanaume. Tume Huru ya Uchaguzi ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza majimbo ya uchaguzi.
Rasimu ya Kwanza ilitaja mikoa kwa Tanzania Bara na wilaya kwa Zanzibar kama  majimbo  ya  uchaguzi. Hoja iliyojitokeza  wakati  wa  kutoa maoni  kuhusu Rasimu hii ni uwezekano wa majimbo kubadilika kwa kuwa tawala za mikoa si suala la Muungano. Rasimu ya pili inaleta utata  zaidi  kwa  kutaja  idadi ya wabunge  na kuipa  Tume  Huru ya Uchaguzi mamlaka ya kugawa na kutangaza majimbo ya uchaguzi. Wakati katika Rasimu ya Kwanza  ilikuwa rahisi kujua kwamba mikoa au wilaya ingekuwa kianzio cha kuunda  majimbo, ibara hii ya Rasimu ya Pili haitoi kiashiria chochote cha aina hiyo, kwakuwa nchi washirika zitakuwa na mabunge yao na utaratibu wao wa kugawa rnajimbo ni vigumu kutabiri namna Tume hii itakavyofanya kazi  yake  kwa murua  katika  nchi washirika  na Tume zake za uchaguzi.
Suraya17
Sura hii ni mpya. Inahusu mambo ya mpito ambayo yatashughulikiwa  katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia Aprili 2015 hadi 31 Desemba 2018.
Utaratibu wa kuwa na kipindi cha mpito ni wa kawaida katika mabadiliko ya aina hii. Rasimu inaleta mapendekezo makubwa mno ambayo yatabadilisha kabisa sura ya taifa letu. Muda wa mpito ni mfupi sana,  kwani ni katika kipindi hicho baadhi ya
7
 mabadiliko yatokanayo na   muundo wa serikali tatu yanatakiwa yawe yamekamilika. Kwa mfano:
·         Katiba ya Tanganyika kuundwa;
·         Katiba ya Zanzibar kubadilishwa ili iakisi mapendekezo ya mundo wa serikali tatu;
·         Kugawana raslimali na madeni kati ya serikuli ya Muungano, Zanzibar na Tanganyika;
·         Kutunga na kurekebisha sheria mbali mbali za nchi washirika ili kuwiana na Katiba mpya;
·         Mgawanyo wa watumishi wa umma;
·         Kuundwa kwa Tume na taasisi za kikatiba zilizoainishwa kwenye Rasimu.
Mambo yanayoelezwa katika sura hii pamoja na kulenga kipindi cha mpito, yanaonesha kwamba hata gharama za muundo huu hazitabiriki. Vile vile katika kipindi hicho cha.mpito kuna hatari ya mipango mingi ya.kushughulikia matatizo ya wananchi kusimama.
 4. MAPENDEKEZO, AMBAYO HAYAKUZINGATIWA NA, AMBAYO BADO YANAHITAJI KUTAZAMWA UPYA
Katika Rasimu ya Kwanza CCM ilizitolea mapendekezo lbara kadhaa  arnbazo tuliona ni vema zikaangaliwa kwa madhumuni yafuatayo:
·         Kupata mtiririko mzuri wa maudhui ya Katiba ili iwe nyepesi kueleweka. Hili   lilikuwa   rnuhimu   kama   sehemu ya kuifanya iwe kweli Katiba ya wananchi kwa ufasaha na matumizi yake. Kwa mfano:
·         Ibara za 52; 53, 54 na 55 ambazo zilikuwa ibara za 50, 51, 52 na 53 mtawalia katika Rasimu ya Kwanza zina vipengele vingi vinavyohusu haki ya binadamu. Ilipendekezwa ibara hizi zifupishwe na zirudishwe katika Suraa ya Nne ya Rasimu inayohusu Haki za Binadamu. Pendekezo hili halijazingatiwa. Lengo ni kuwa na mtiririko mzuri wa vifungu vya Katiba ili mambo yanayofanana yakae sehemu moja.
·         Katiba ni sheria kuu na utamaduni unaozingatiwa duniani kote ni kuifanya iwe rahisi kueleweka lakini ni vigumu kuibadilisha. Rasimu hii kama ilivyokuwa Rasimu ya Kwanza imebeba mambo mengi mno na yanayokwenda kwa kina mno kwa sheria kuu. CCM inaamini bado ipo haja kwa  Rasimu  ya  Tatu  kuzingatia  suala  hili  ili  yale  ambayo yanaweza kutungiwa sheria, ifanyike hivyo. Sheria za kawaida ni rahisi zaidi kuzifanyia marekebisho kuliko Katiba. Kwa mfano:
8
           
Ibara  ya  43 ambayo ilikuwa ibara ya  42 katika Rasirnu ya  Kwanza. CCM ilipendekeza haki za mtato zitajwe kimsingi katika Rasimu lakini zianishwe kwa  ufasaha  katika  Sheria  ya  Mtoto. Pendekezo  hili halijazingatiwa. Ukweli ni kwamba haki za mtoto zinaweza kubadilika, kuimarishwa au kuongezwa, jambo ambalo litafanyika kwa urahisi kwenye sheria ya kawaida, tofauti na Katiba ambayo ina utaratibu  mrefu  na  mgumu  wa kuifanyia marekebisho. Hii pia  itaondoa  wingi  wa  ibara  kwani  kwa  asili yake  Katiba  ilipaswa  kubeba  mambo  makuu  na  ya  msingi  ili  yawe  dira katika sheria nyingine.
Mifano hii inaonesha kuwa mapendekezo ya CCM yalilenga kuona kwamba Katiba inaweka misingi na ulinzi madhubuti wa jumla wa haki za binadamu ili baadaye zifafanuliwe vizuri katika sheria mbalimbali za nchi. Hii itaepusha kuweka mambo mengi mno kwenye Katiba, na pia italeta urahisi endapo sheria itahitaji marekebisho, tofauti na Katiba ambayo utaratibu wa kuirekebisha ni mrefu na mgurnu. Maoni mengine ya CCM ambayo hayakuzingatiwa yalihusu ibara zifuatazo:
Ibara ya 2
 CCM ilipendekeza maneno katika ibara hii yasomeke ''eneo lote la Tanzania Bara na
eneo lote la Zanzibar pamoja  na sehemu zake zote za bahari, maziwa,  rnito na maeneo rnengine yatakayoongezwa" Maneno: "Maziwa, mito na maeneo mengine yatakayoongezeka” hayajazingatiwa.
Maeneo ya ndani yenye maji ambayo ni sehemu ya nchi yasipotajwa bayana kunaweza kuwa na changamoto ya tafsiri ya mipaka kati ya nchi yetu n anchi nyingine jirani. Kwa mfano pale mpaka rmapopita juu ya maji mfano mgogoro unaotaka kujitokeza kuhusu umiliki wa Ziwa Nyasa.
Ibara ya 10
Hii ilikuwa ibara ya 11 katika Rasimu ya Kwanza ikihusu malengo makuu ya Serikali
na utekelezaji  wake.  CCM ilikuwa na maoni kwamba  kutokana Muundo wa Serikali unaopendekezwa malengo haya hayawezi kutekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano bali nchi washirika.
Malengo yanayotajwa yako katika maeneo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, kisiasa hususan katika ngazi ya kijamii na kimazingira. Hata hivyo kwa mundo wa Muungano unaopendekezwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano haina mamlaka wala madaraka ya kuyashughulikia mambo haya kwa sababu si mambo ya Muungano.
Ibara 11(2)
Ibara hii inahusu Serikali kutakiwa kutoa tarifa Bungeni si chini ya mara moja kwa mwaka kuhusu utekelezaji wa malengo haya.
9
Muundo wa serikali tatu unaopendekezwa hautaliwezesha Bunge la Muungano kuhoji utekelezaji wa malengo haya kwa sababu yatakuwa kwenye himaya ya washirika wa Muungano, ambapo malengo yatajadiliwa kwenye mabunge yao.
Ibara ya 84 na 85
Ibara hizi zilikuwa  za 80 na 81 kwenye Rasimu ya Kwanza mtawalia. CCM ilipendekeza ibara hizi ziangaliwe upya kwa kuzingatia mapendekezo ya mundo wa serikali mbili.
Pendekezo hili halikuzingatiwa
Hali ya hatari na vita katika nchi ni jambo zito na ndiyo maana kuwekwa kwenye Katiba. Kwa mujibu wa orodha ya Mambo ya Muungano ya 1964 na orodha iliyoko sasa kwenye Katiba ya 1977, hali ya hatari ni jambo la Muungano. Rasim ya Pili imeliondoa kwenye orodha ya mambo ya Muungano. Tafsiri iliyo wazi ni kuwa Rais wa Muungano hana mamlaka ya kutangaza hali ya hatari popote ndani ya Muungano kwani mambo ya hali ya hatari si jambo la Muungano tena.
lbara ya 233 na 234
Ibara hizi zilikuwa ibara za 217 na 218 za Rasimu ya Kwanza mtawalia na CCM ilipendekeza ziboreshwe na 217(1) iongezwe kipengele € chenye maneno “kuandaa na kusimamia sera za kifedha na sera za kibajeti.” Vilevile ilipendekezwa katika ibara ya 213 majukumu hayo yaondelewe kutoka Benki nyinginezo.
Pendekezo hili halijazingatiwa.
Moja kati ya kazi za Benki Kuu ni kusimamia mfumo mzima wa benki za biashara katika nchi. Rasimu ya Pili ibara ya 234 inatoa mamlaka kwa benki za washirika kuhifadhi fedha za serikali zao na kusimamia sera za fedha za benki hizi. Haya ni mamlaka ya Benki Kuu kupanga viwango vya riba, kudhibiti mfumuko wa bei, kusimamia viwango vya kubadilisha fedha za kigeni na masuala mengine yanayohusu sera za kifedha. Pia Rasimu katika ibara ya 233(2) inaeleza kuwa Benki Kuu itakuwa huru katika kufanya kazi zake. Lakini ibara ya 233(3) inasema itatungwa sharia itakayoweka muundo utakaozingatia uwakilishi wa pande zote za Muungano, mamlaka, shughuli na utendaji wa Benki. Uhuru wa Benki hii utakuwa mashakani kutokana na utekelezaji wa ibara hii ndogo yay a 233(3).
  
10
SEHEMU YA PILI
CHANGAMOTO ZA SURA YA SITA
1.   MUUNDO WA MUUNGANO
Eneo kubwa ambalo halikuzingatiwa ni Sura ya Sita ya Rasimu ya Kwanza ibara za 60-69 zilizohusu muundo wa Muungano. Muundo wa Muungano ndiyo moyo wa Rasimu na ndiyo unaoamua ibara nyingine zikae vipi. Kwa hiyo haishangazi kwamba maoni mengi ya CCM katika Sura hii yalikataliwa kwani CCM ilipendekeza muumdo wa sasa wa serikali mbili uendelee.
Mapendekezo ya CCM kuhusu muundo yanatokana na sera yake, lakini ieleweke wazi kwamba hii si sababu peke. Katika maoni yake kwenye Rasimu ya Kwanza CCM iliainisha  sababu  kadhaa  za  kiuchumi,  kijamii,  kisiasa  na  kiusalama  ambazo zina maslahi mapana zaidi kwa taifa letu kuliko sera yake. CCM inaendelea kuamini kuwa mfumo wa serikali mbili ni bora zaidi na unajenga mazingita mazuri zaidi ya kuimarisha Muungano    wetu            endapo    yale    yanayoleta     kero    hivi    sasa yatashughulikiwa kikamilifu na kwa dhati. Uchambuzi wetu wa Taarifa ya Tume na viambatisho vyake unaonesha kwamba yapo mambo makuu mawili ambayo ndiyo msingi wa pendekezo la muundo wa serikali tatu. Kwanza ni malamiko ya pande zote mbili za Muungano na pili ni rnfululizo wa matukio yaliyosababisha mgongano wa Katiba.
(i)     Malalamiko
Kwa upande wa Zanzibar malalamiko yanayotajwa:
·         Kuondolewa kwa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano;
·         Kuongezeka   kwa  mambo  ya  Muungano na  hivyo  kuathiri madaraka ya Zanzibar   (autonomy)   na   kufifisha    utambulisho (identity) wake na Zanzibar kuendelea kumezwa;
·         Hisia kuwa Tanzania Bara imevaa koti la Serikali ya Jamhuri ya Muungano na hivyo kutumia mamlaka hayo kujinufaisha yenyewe kwa gharama ya Zanzibar; na inafanya hivyo kwa kutobainisha marnlaka ya Serikali ya Muungano kwa mambo yaliyo ya Muungano   kwa   upande  mmoja;  na mamlaka   hayo   hayo  kwa mambo yasiyo ya Muungano kwa upande mwingine;
·         Mkanganyiko kuhusu ugawaji wa mapato na jinsi ya kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli za Muungano vaina ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.
11
Malalamiko ya Tanzania Bara
·         Zanzibar imekuwa nchi huru, ina bendera yake, ina wimbo wake wa Taifa, ina Serikali yake na imebadili Katiba yake ili ijitambulishe kama nchi, wakati Tanzania Bara imepoteza utambulisho wake. Katiba ya Jamhuri inasema Tanzania ni nchi moja lakini Katiba ya Zanzibar inasema ni nchi mbili;         
[Ibara ya (1) inatamka “Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake…”; Ibara ya (2) ya Katiba ya Zanzibar inasomeka: “Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano ya Tanzania]
·         Zanzibar imebadili Katiba yake na kuchukua madaraka ya Jamhuri ya Muungano, kama kama vile kuelekeza sharia za Muungano zilizopitishwa na Bunge la Muungano zipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi. Maana yake ni kuwa Katiba ya Zanzibar sasa ipo juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano;
·         Ushiriki wa wabunge wa Zanzibar katika kujadili na kupitisha sheria kwa masuala yasiyo ya Muungano ndani ya Bunge na kwa wabunge wa Zanzibar kuwa mawaziri kwa masuala yasiyo ya Muungano; na
·         Haki ya kumiliki ardhi – wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati wenzao wenzao upande wa Zanzibar waba haki hiyo Tanzania Bara.
(ii)   Mgongano wa Katiba
Hoja ya pili inayochukuliwa kama sababu ya kutaka serikali tatu ni migongano iliyopo kati ya Katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano, ni upande wa Serikali ya Muungano kutotimiza majukumu yake kikatiba. Utafiti uliofanywa na Tume kuhusu masuala yanayogusa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unabainisha maeneo yafuatayo yenye migongano ya kikatiba:
a.      Katiba ya Zanzibar
Mamlaka ya Dola
Ibara ya (i) ya Mkataba wa Muungano wa mwaka 1964 iliainisha kuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa nchi moja  yenye mamlaka moja ya kidola. Vile vile Ibara ya 1 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inatamka kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja. Hata hivyo ibara ya (1) ya Katiba ya Zanzibar inatamka kuwa Zanzibar ni nchi. Tume inaonesha kuwa ibara hii ya Katiba ya Zanzibar inakinzana na Katiba ya Muungano kwa kuwa Jamhuri ya Muungano ni nchi moja na dola moja.
12
Majeshi ya Ulinzi na Usalama
Ibara ya 147 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imekataza mtu yeyote au shirika au kikundi cho chote kuunda na kuweka Jeshi katika Tanzania isipokuwa Serikali ya Jamhuri ya Muumgano pekee yenye mamlaka ya kuunda majeshi ya Ulinzi na Usalama. Katiba ya Zanzibar, kupitia ibara ya 12 1imeanzisha idara maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zikiwemo "Jeshi1a Kujenga Uchurni (JKU), Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) na Chuo cha Mafunzo (cha wahalifu). Kwa mujibu waTume, Katiba ya Zanzibar inakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa kuanzisha majeshi wakati hilo ni jukumu la Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Utungaji wa Sheria za Muungano
Ibara ya 64(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inalipa mamlaka Bunge Ia Muungano kutunga sheria ambazo zinaweza kutumika Zanzibar. Katiba ya Zanzibar, ibara ya 132(1) inaweka masharti ya kutumika kwa sheria iliyotungwa na Bunge  la Muungano kwa kutaka  sheria hiyo iwe ni kwa  ajili ya  mambo ya Muungano tu. Ibara ya 132(2) inafafanua kwamba Sheria hiyo lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika. Tume inaeleza kuwa hali hii inaleta mgogoro wa kikatiba.
Mahakama ya Rufani
Wakati Mahakama ya Rufani, kwa mujibu wa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni mahakama yenye uwezo wa kuamua rufaa zote nchini, ibara ya 99 ya Katiba ya Zanzibar inatakata mtu yeyote yule wa Zanzibar kupeleka kwenye Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesi zozote zinazohusu tafsiri ya Katiba ya Zanzibar, mambo ya Kiislamu ambayo yameanzia katika Mahakama ya Kadhi na mambo mengine yoyote yaliyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar na sheria nyingine yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi. Ibara hii inaonekana kukinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mamlaka ya Mahakama ya Rufani.
Mamlaka ya Kugawa Mikoa
Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano kugawa mikoa nchini. Wakati huo huo, Katiba ya Zanzibar inampa Rais wa Zanzibar mamlaka kama hayo na hivyo kukinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
b.      Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Katiba
Kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Tume katika Ripoti yake inabainisha maeneo kadhaa ambayo yameleta mkanganyiko katika
13
utekelezaji wa katiba, lakini haikutamka bayana kwamba mkanganyiko huo ni matokeo ya Katiba kutozingatiwa kikamilifu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Kutotenganisha Mambo ya Tanzania Bara na ya Jamhuri ya Muungano
Ibara ya 34 ya Katiba ya mwaka 1977 inaainisha mambo ambayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano itaakuwa na mamlaka nayo. Ibara hiyo inafafanua wajibu wa Serikali ya Muungano kwa mambo ya muungano na mambo yasiyo ya muungano yanayohusu Tanzania Bara.
Ilitarajiwa kwamba ibara hii ingetekelezwa kwa Serikali ya Muungano kuweka wazi mipaka yake, wakati gani inasimamia mambo ya Muungano na wakati gani inasimamia mambo ya Tanzania Bara. Matokeo yake ni malalamiko kwamba Tanzania Bara imevaa koti la Serikali ya Jamhuri ya Muungano na hivyo kutumia mamlaka hayo kujinufaisha yenyewe kwa gharama ya Zanzibar. Kushindwa kutenganisha mipaka hiyo ni mojawapo ya kero za Muungano.
Uundaji wa Tume ya Pamoja ya Fedha na Akaunti ya Fedha ya Pamoja
Ibara ya 133 inaitaka Serikali ya Muungano kuanzisha Akaunti ya Fedha ya Pamoja (Joint Finance Account). Lakini akaunti hii haijaanziswa na hivyo kuwa sehemu ya manung’uniko ya Zanzibar na Zanzibar kushindwa kuchangia matumizi ya Muunagano na kushindwa kufaidika na mapato ambayo yangetokana na akaunti hii.
Ibara ya 134 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano iunde Tume ya Pamoja ya Fedha (Joint Finance Commission). Tume hii ilichelewa sana kuundwa. Tume ilizinduliwa mwaka 2003, lakini haikufanya kazi hadi mwaka 2006 ambapo jukumu lake la kwanza lilikuwa ni kufanya uchambuzi wa masuala mbali mbali ya Muungano na kuyatolea mapendekezo Serikalini. Mapendekezo hayo vado hayajafanyiwa kazi kwa mujibu wa hadidu za rejea.
MUUNDO WA SERIKALI TATU UTAJIBU CHANGAMOTO HIZI?
Malalamiko ya migongmo  iliyoainishwa ina uzito wake.  Changamoto  hizi zimekuwepo   kwa muda  mrefu  na  kumekuwa na jitihada za mara kwa mara kuzikabili. Tume na kamati mbali mbali ziimejishughulisha kutafuta ufumbuzi. Kumekuwa na hoja kwamba Tume na Kamati nyingi za nyuma zilitoa pendekezo la serikali tatu na hivyo sasa wakati umefika wa kuzingatia mapendekezo hayo. Je, baadhi ya Tume na Kamati za nyuma zilisemaje? Tume ya Nyalali ilikuwa na wajumbe 22, wajumbe 13 walipendekeza muundo wa serikali tatu, wajumbe 9 hawakuafiki mundo huu. Kamati ya Jaji Kisanga ilikuwa na wajumbe 15 ambapo 12 walipendekeza muundo wa Serikali tatu na 3 walitaka muundo wa serikali mbili
14
uendelee. Kwa kuangalia mtiririko huu imejengeka dhana kwamba Tume nyingi zimmetoa mapendekezo hayo na wananchi wanataka hivyo. Lakini hata kalika Tume na Kamati hizi hakukuwa na makubaliano ya moja kwa rnoja.   .
Swali ambalo CCM inajiuliza, je, mundo wa serikali tatu utajibu changamoto za Muungano? CCM haiamini hivyo, kwani kwa maudhui yake Rasimu ya Pili ina
uwezekano mkubwa wa kuendeleza changamoto zile zile, kuzua mpya au nyingine nyingi zaidi ambazo zitadhoofisha Muungano wetu. Changamoto hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:
(i)     Ukuu wa Katiba na tekelezaji wa sheria
Maoni yetu ni kwamba Katiba ni waraka wa kisheria, matukio yote yaliyochukuliwa kama sababu ya pendekezo la muundo wa serikali tatu yanatokana na Katiba kutozingatiwa. Hatuamini kwamba idadi ya serikali ndiyo itakuwa tiba endelevu kama hakutakuwa na misingi madhubuti ya kuheshimu Katiba. Kama Katiba haizingatiwi, hilo litadhoofisha Muungano wowote ule, uwe wa serikali mbili au tatu.
Kwa kuzingatia umuhimu wa Katiba kuheshimiwa Tume inapendekeza kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano:
·         itamke bayana kuwa Katiba ya Muungano ndiyo itakuwa na nguvu kuliko Katiba zingine. Kwahiyo Katiba ya mshirika wa Muungano ikikinzana na Katiba ya Muungano basi itakuwa ni batili;
·         itamke kuwa ikianza kutumika ni lazima Washirika wa Muungano wabadilishe Katiba zao ndani ya muda Fulani ili ziweze kuendana na Katiba ya Muungano.
Mapendekezo haya yanayohusu ukuu wa Katiba si mapya. Katiba ya 1977 ina vipengele hivyo hivyo na huenda vilivyokaa kimadhubuti zaidi ya hivi vilivyopendekezwa na Tume. Ni wazi kwamba tatizo si kutokuwepo kwa vipengele vinavyohusu ukuu wa Katiba.  Kwani  migongano  mingi iliyotokea haikusababishwa na ukosefu wa ibara zinazohusu ukuu wa Katiba bali Katiba yenyewe kutozingatiwa.
Hali kadhalika masuala mengine yenye utata wa kikatiba au kisheria yanaweza kushughulikiwa na mfumo uliopo ndani ya Katiba yenyewe. Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaunda Mahakama Maalum ya Katiba ambayo ina jukumu la kusikiliza na kusuluhisha suala lolote linalohusu tafsiri ya Katiba.
Mamlaka ya Mahakama hii yanaweza kupanuliwa ili iweze kushughulikia changamoto ambazo zina sura ya mgongano wa kikatiba au kisheria. Kwa mfano mgongano ulioelezwa kuhusu uundwaji wa majeshi ya ulinzi na usalama, ungeweza ukatatuliwa kupitia Mahakama hii. Kuundwa jwa vikosi kama JKU, KMKM na
15
Chuo cha Mafunzo kulifanywa kwa sababu maalum. JKU iliundwa kuhamasisha shughuli za kiuchumi na za kijamii hasa kwa vijana. KMKM kuzuia magendo ya karafuu na Chuo   cha   Mafunzo   kwa   ajili   ya   kurekebisha   mwenendo  wa watu waliotiwa hatiani (ni kama idara ya magereza kwa Zanzibar).
Kwa hiyo kama kuna utata wowote kuhusu hadhi ya vikosi hivi kwa namna vilivyoanzishwa au jinsi vinavyoendeshwa hivi sasa, basi Mahakama hii ingeweza kabisa (ikiwa na mamlaka iliyoimarishwa) kuamua kama vikosi hivi vina sura ya uanzishwaji wa majeshi kwa namna inayokatazwa  na ibara ya 147 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977. Kwa mantiki hii, suluhisho si idadi ya serikali bali mfumo wa kisheria wa kushughulikia masuala haya.
(ii)   Changamoto za kimfumo na kitaasisi katika mfumo unaopendekezwa
·         Kiutawala na kwa mamlaka iliyopewa na Rasimu, Serikali ya Muungano imeundiwa mfumo ambao unaitenganisha na wananchi, kwani  serikali hiyo haina mamlaka ya kushughulikia masuala yanayowagusa moja kwa moja. Masuala kama elimu, kilimo, maji, yote yamo kwenye mamlaka ya washirika wa Muungano. Hali kadhalika Rasimu inatamka kuwepo kwa Mawaziri Wakaazi (ibara ya 67) ambao jukumu lao ni kuratibu na kusimamia mahusiano vaina ya Serikali z anchi washirika; na kati ya Serikali ya nchi mshirika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
·         Rasimu inaunda Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali itakayokuwa na jukumu maalum la kuwezesha uratibu na utekelezaji wa masharti ya Katiba, será, sheria na mipango baina ya Serikali ya Muungano na serikali za nchi washirika na baina ya serikali za nchi washirika. Kuwepo kwa vyombo hivi kunaongeza matabaka mapya na mengi ya urasimu na hivyo kuzidi kuiweka Serikali ya Muungano mbali na wananchi.
·         Rasimu ya Katiba imetoa jukumu kwa viongozi wakuu wa Muungano n anchi washirika kuulinda Muungano. Hili ni lengo zuri lakini Rasimu ilipaswa kwanza kuweka mundo madhubuti wa Muungano ambao ndiyo ungekuwa msingi wa kuulinda. Badala yake Rasimu inaunda Muungano dhaifu ambao unaonyesha dalili nyingi za kuvunjika huku ikiaminika kwamba marais watatu wanaweza kuulinda usivunjike.
·         Rasimu imeondoa mundo wa Serikali ya Muungano w anchi mbili na kuleta shirikisho la serikali tatu, ambalo linadhoofisha Muungano;
·         Rasimu imepunguza orodha ya mambo ya Muungano bila kuangalia taathira yake kwa nchi. Hatua ya kupunguza mambo ya msingi yanazileta nchi zilizo kwenye Muungano pamoja haiwezi kuhesabiwa kama inaimarisha
16
Muungano. Kwa mfano Ulinzi na Usalama ni jambo la Muungano lakini mawasiliano, usafiri wa anga na bandari si mambo ya Muungano. Katika hali hii nchi haiwezi kuwa na ulinzi madhubuti kama haidhibiti mawasiliano, usafiri wa anga na bandari.
·         Uraia unachukuliwa kuwa ni jambo la Muungano. Lakini mfumo wote unaopendekezwa unajenga mazingira ya “kila mtu kuchukua chake” kwa namna ambayo unaweza ukazua será za ukaazi, ardhi na biashara ambazo hazitalazimika kufuata tunu za Muungano kama vile umoja. Mfumo huu utaibua kwa urahisi dhana ya “Utanganyika” na “Uzanzibari”, ambazo zitachukua nafasi ya “Utanzania”. Na hivyo kuuweka mashakani umoja na utangamano wa taifa letu.
Uchambuzi wetu wa sababu zinazotumiwa kuhalalisha  serikali .tatu unaonesha kwamba changamoto za mfumo mpya ni nyingi na ngumu zaidi kuliko mundo wa serikali mbili.
(iii) Changamoto za gharama za uendeshaji wa Serikali ya Muungano
Mojawapo ya mambo ambayo yanahitaji kutazamwa kwa kina katika mundo unaopendekezwa ni gharama za kuendesha Serikali ya Muungano, lakini pia athari za gharama hizi kwa nchi washirika. Rasimu inaainisha vyanzo vya mapato katika ibara ya 231 ya Rasimu kuwa:
·         ushuru wa bidhaa;
·         mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na taasisi za Muungano;
·         mchango kutoka kwa nchi washirika;
·         mikopo kutoka ndani na  nje ya Jamhuri ya Muungano; na
·         mapato mengine.
Ushuru wa bidhaa ni ushuru unaotozwa katika bidhaa mbali mbali ili kuongeza mapato (bidhaa kama soda, bia, vinywaji vikali, maji ya matunda au huduma za simu za mkononi) au wakati mwingine kupunguza matumizi ya bidhaa Fulani Fulani (kama mifuko ya plastiki, sigara na nyinginezo).
Chanzo hiki ni mojawapo ya vyanzo vya kugharimia uendeshaji wa Serikali ya Muungano. Hata hivyo Serikali ya Muungano haina sekta za kiuchumi ambazo zinazalisha. Kwahiyo kodi inayoelezwa ni ile iliyo ndani ya será zakodi z anchi washirika na ambayo itakusanywa na nchi washirika wenyewe, lakini wanalazimika kuiwasilisha kwenye Serikali ya Muungano. Haifahamiki makusanyo hayo yatatosheleza kiasi gani lakini uzoefu uliopo wa bajeti ya Serikali ya Muungano, unaonyesha kwamba kiasi cha ushuru wa bidhaa kinachokusanywa hakilingani na majukumu ya serikali kwani ni kidogo. Kwa mfano, wakati makadirio ya matumizi kwenye mambo ya Muungano yaliyoainishwa na Rasimuni kiasi cha shilingi trilioni 2.354, makusanyo ya ushuru wa bidhaa kwa mwaka 2012/2013 yalikuwa kiasi cha shilingi trilioni 1.3.
17
Chanzo kingine cha mapato kinachotajwa ni mchango w anchi washirika. Katika eneo hili Rasimu inatoa mwongozo uchangiaji huu utafanyika vipi na kwa uwiano gani.  Huu ni upungufu unaofanana na tatizo lililokuwepo kwa muda mrefu katika Katiba ya mwaka 1977, lililohusu kutoanzishwa kwa Akaunti ya Pamoja ya Fedha na utaratibu wa kuchangia na kugawana mapato ya Muungano. Mwongozo huu ni wa muhimu sana kutokana na mambo mawili. Rasimu inasema kwamba washirika wa Muungano watakuwa na hadhi sawa [ibara ya 64(4)]. Hii inaweza kueleweka kwamba mchango w anchi washirika utakuwa sawa kwa sawa. Hata hivyo ukweli ulio wazi ni kwanza uchumi wa Tanganyika ni mkubwa kuliko ule wa Zanzibar. Kwahiyo kama suala hili halijaeleweka vizuri ndani ya Katiba litakuwa ni chanzo cha kutoelewana na kuudhoofisha Muungano.
Suala jingine linalohusu chanzo hiki cha mapato ni kwamba washirika watatakiwa kuchangia tena kwenye Serikali ya Muungano wakati ambapo tayari chanzo chao kingine (ushuru wa bidhaa) kimeshatolewa kwa Serikali ya Muungano kama Katiba Inavyotaka. Hii italeta manung'uniko mapya hasa kutoka Zanzibar ambayo uchumi wake mdogo utaathirika zaidi kuliko wa Tanganyika. Hapana shaka  kwamba kwa ujumla wake mundo huu unaopendekezwa utaongeza gharama kwa nchi washirika.
Vilevile, Rasimu inaainisha mikopo toka ndani na nje kama chanzo kingine cha mapato kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, kwa mujibu wa orodha ya mambo ya Muungano Serikali ya Muungano haitajishughulisha na uzalishaji wenye faida ya kipato na haina raslimali zozote za kiuchumi (investable resources). Kwa hali hiyo haikopesheki ndani wala nje ya nchi. Hii ni kwa sababu mambo ya Muungano yote ni ya huduma kwa wananchi (Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania; Ulinzi na Usalama; Uraia na Uhamiaji; Sarafu na Benki Kuu; Mambo ya Nje; Usajili wa Vyama vya Siasa; ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na mambo ya Muungano).
Kwa upande wa mapato yasiyokuwa ya kodi yatokanayo na taasisi za Muungano kikubwa kinachotegemewa hapa ni maduhuli (kama vile malipo ya viza kwa wageni wanaoingia nchini; malipo ya kuanzisha kampuni na mengineyo) ambayo ni kiasi kidogo sana cha fedha. Hivyo basi, kwa kuzingatia kodi itokanayo na ushuru wa bidhaa ni ndogo, maduhuli pia ni kidogo, Serikali ya Muungano haitaweza kujiendesha  kwa vyanzo hivi ambavyo ndivyo vinaonekana kupewa kipaumbele.
Rasimu vile vile inabainisha kuwa Serikali ya Muungano itakuwa na vyanzo vya mapato ambavyo havijaainishwa kwa kusema "mapato mengine." Chanzo hiki hakieleweki kwani Rasimu haijaweka wazi hayo mapato mengine ni yepi. Chanzo chochote cha mapato lazima kielezwe vizuri kwani mapato siyo tu suala la kodi bali  la kisheria, na mazingira ya kupatikana na kutozwa kwake lazima yafahamike  wazi kwa wanaotozwa.      
Kwa ujumla, ni wazi kwamba gharama za kuendesha Serikali ya Muungano zitakuwa ni kubwa kuliko mapato.ya Muungano kama tulivyoonesha hapo juu. Na
18
bado haijulikani  uendeshaji wa taasisi nyingine utakuwaje ambazo zitahusika na usimamizi wa baadhi ya mambo ya Muungano kwa upande mmoja, na kughalimia vyombo muhimu kama vile Ofisi ya Rais wa Jamhuri wa Muungano, Bunge la Jamhuri ya Muungano; chombo cha kusimamia manunuzi ya umma; chombo cha uendeshaji wa Mfuko Mkuu wa Hazina; chombo cha kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali ya Muungano; Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali na taasisi nyingine nyingi zitakazoundwa.
Hivyo basi, muundo unaopendekezwa na Rasimu utakuwa na gharama kubwa sana za uendeshaji kuliko vyanzo vya mapato vilivyoaninishwa.
 19
SEHEMU YA TATU
HITIMISHO NA MWELEKEO
CCM inatambua changamoto zilizoainishwa na umuhimu wa kuzishughulikia kwa njia endelevu kwa kutumia Katiba, sheria na taratibu za uendeshaji. Mapendekezo yetu ya kuendelea na mfumo wa serikali mbili hayatokani tu na será ya CCM, bali udhaifu mkubwa uliojionesha katika pendekezo la mundo wa serikali tatu. Hivyo basi CCM inapendekeza kwamba mfumo wa serikali mbili ufanyiwe marekebisho ambayo yatashughulikia changamoto zilizopo. Marekebisho hayo ni pamoja na kuzingatia:
yetu ya kuendelea na•n-.ft.uno wa serikali mbiii h.c1yr.:o:.:mi tll na sera ya CCM, bnli udhaifu mku"bwa dicjione:;ha katika pendekezo Ja znuunJo wa: serikali tatu. Hivyo basi cc.M U16.pendekeza kwiunba Infumo wa 5CiikaU mbU.i u{imyi\ve•\iuirekibisho ambayo yatashii:ghu!iki ch.angamoto ilizop . ]..1arel
1.      Nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Muungano
Rais wa Zanzibar awe Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa msaidizi wake kwa masuala ya Zanzibar na mmoja wa viongozi wakuu wan chi. Hii itaongeza kuweka wazi madaraka ya Rais wa Zanzibar ndani ya Serikali ya Muungano na nje ya nchi.
2.      Akaunti ya Fedha ya Pamoja
Ifunguliwe Akaunti ya Fedha ya Pamoja ambamo zitawekwa fedha zote zitokanazo na mapato ya vyanzo vya Muungano kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Aidha, uwepo utaratibu wa kisheria utakaoelekeza uendeshaji wa akaunti hii pamoja na kuweka mgawanyo wa mapato hayo kwa pande mbili za Muungano. Hii itasaidia kuwianisha uchumi wa pande hizo mbili. Sheria kuhusu utaratibu huu isimamiwe na Tume ya Uhusiano na Uratibu kama ilivyoperidekezwa katika Rasimu.
3.      Tume ya Pamoja ya Fedha
Tume hii ambayo imetamkwa  kwenye Katiba na kwa kupitishwa na sheria ya Bunge imeshaundwa hivi sasa, na mamlaka yake yanafahamika. Tunapendekeza tume hii ipewe nguvu zaidi , iwekewe mfumo madhubuti wa kuendesha na kusimamia kwa karibu. Mapendekezo yanayotolewa na Tume yashughulikiwe na serikali zote mbilikwa haraka , ili kama hakuna kikwazo mapendekezo yake yatekelezwe bila kuchukua muda mrefu.
4.      Sheria mahususi kuhusu Uratibu wa Mambo ya Muungano
Iwepo Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano kikatiba na uendeshaji wake ulingane na mwenendo wa sasa wa vikao vya pamoja vya kero. Uratibu na usimamizi wa masuala ya Muungano uwekwe kisheria na Tume ipewe mamlaka ya kuzisirnamia taasisi zote za Muungano katika makubaliano yatakayoafikiwa na pande zote mbili.                         
20
5.      Uhusiano wa kimataifa na mashirika/taasisi za nje
Zanzibar iweze kuwa na uhusiano wa kimataifa katika masuala yasiyo ya Muungano, kwa kuihusisha Wizara ya Mambo ya Nje.
6.      Uwezo wa Zanzibar kukopa ndani na nje
Katika maeneo ambayo si ya Muungano Zanzibar iwe huru kutafuta misaada na mikopo yenyewe bila vikwazo ila Wizara za Fedha na Mambo ya Nje zishirikishwe.
7.      Kutenganisha mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano
Ili kuondoa rnkanganyiko  wa  Tanzania  Bara  kuvaa  koti  la  Serikali  ya Muungano, tunapendekeza mabadiliko katika vyombo vya Muungano:
(i)           Bunge       
·         Pendekezo la kwanza: kuwe na Baraza la Wawakilishi la Tanzania  Bara kwa ajili ya kushughulikia masuala ya Bara tu. Katika pendekezo hili majimbo ya Jamhuri ya Muungano yaundwe upya  ili majimbo ya uchaguzi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar yawe ndiyo hayo hayo majimbo ya uchaguzi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.
·         Endapo muundo huu utaafikiwa basi masuala ya Muungano yatakuwa yakitekelezwa na Bunge litakalowashirikisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar (ambao watatumika kama wajumbe wa Bunge la Muungano na Wabunge wa Tanzania Bara (ambao watashughulikia masuala ya Tanzania Bara katika Baraza lao la Wawakilishi)).
·         Pendekezo la pili: Bunge  la Muungano wakati linajadili mambo ya Muungano wabunge wote washiriki majadiliano na itapofikia kujadili mambo ya Bara washiriki wabunge wanaotoka Bara tu. Kama  Spika anatoka sehemu moja ya Muungano, Naibu wake atatoka upande wa pili na wakati wa vikao vya masuala ya Bara Spika/Naibu Spika anayetoka Bara ndiye atakayeendesha kikao. Inapendekezwa Bunge la Jamhuri ya Muungano liwahusishe Wabunge w apande zote za Muungano linapojadili masuala ya Muungano. Kwa mambo yanayohusu mambo yasiyo ya Muungano, haya yatekelezwe na Wabunge wa Tanzania Bara pekee.
(ii)       Mawaziri Katika Serikaii ya Muungano   
Wajumbe wa Bunge la Muungano wanaweza kuwa mawaziri wa wizara za mambo ya Muungano tu. Wizara zisizo za Muungano ziongozwe na wabunge wanaotoka Tanzania Bara tu.
(iii)    Mambo ya Muungano                                                                                           Pamoja na orodha ya mambo ya Muungano ambayo yatakuwa kwenye Katiba, mambo yasiyo ya Muungano yaorodheshwe kwenye sheria itakayoainisha pia usimamizi, utekelezaji wake na gharama zake.
21
(iv)    Muundo wa Mahakama ya Juu                                                                           Ndani ya Mahakama ya Juu kiwepo kitengo maalum kitakachoshughulikia masuala ya Katiba tu
(v)      Misaada na mikopo nafuu kutoka kwa wahisani
Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zijadili kwa kina kanuni ya mgawanyo wa fedha zinazopatikana  toka chanzo hiki. Kuwekwe utaratibu wa kisheria  kutenganisha misada inayotekelezwa kwenye miradi ya Muungano na isiyo ya Muungano.
 
Source: Maisha Time
 

No comments:

Post a Comment