Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, March 31, 2014

PANONE FOOTBALL CLUB YAZIZIBA MIDOMO TIMU 16 ZA MKOA WA KILIMANJARO

Wachezaji wa Panone FC. wakipasha misuli dakika chache kabla ya kuanza kukabiliana na Machava Fc.

Wachezaji wa Panone FC. na Machava FC. wakisalimiana kabla mechi kuanza.

 Panone FC wakisali kabla ya mechi kuanza.
 Kikosi cha Machava FC kikiwa kinakumbushana mambo muhimu kabla ya mechi kuanza.

 Waamuzi wa Mchezo wakipeana mikono tayari kwa kwenda kuchezesha mechi kati ya Panone FC na Machava FC.

 Benchi la ufundi la Machava FC.

 Benchi la ufundi la Panone FC.

Mchezaji wa Panone FC. Tony Kingundu akiwa chini lakini bado anapa anaumiliki mpira.

 Faulu ikipigwa kuelekea lango la Panone FC.

 Faulu ikipigwa kuelekea lango la Machava FC.

 Kocha wa Panone FC akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
 Kocha wa Machava FC akitoa maelekezo kwa wachezaji wake
Viongozi wa KRFA wakizungumza na wachezaji wa timu zote mbili na kuwasifia kwa mchezo mzuri walio uonesha.

 Faulu ikipigwa kuelekea lango la Machava FC.

 Huyu ni Tonny Kingundu aliyeipatia Panone FC goli na kuwafanya waibuke kidedea.

Hadi Mwisho wa mchezo ubao ulionesha Panone 1 Machava 0
 Panone FC wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushinda.

 Wachezaji wa Panone wakipeana mikono na waliokuwa meza kuu.
 Captain wa timu ya Panone FC, Hamis Chedo akipokea kombe.

 Timu ya Panone ikishangilia ushindi baada ya kukabidhiwa kombe.

Panone and co. ltd ni kampuni ya Usambazaji na uuzaji wa mafuta ya magari jumla na rejareja katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa masaa ishirini na nne kwa wateja wake na katika kila kituo kuna supermarket na huduma ya kibenki na kifedha kupitia M-Pesa inayopatikana muda wote. Panone and Company Ltd, ina bakery ya kisasa ambayo kwa sasa inatengeneza mikate inayokwenda kwa jina la Panone Bread, Queen Cake, Pan Cake, Maandazi na pia inafanya Parking ya Mchele, Korosho, Karanga na vyote hivyo vikiwa katika nembo ya Panone, na pia wanamilikia timu ya mpira wa miguu inayofahamika kama Panone Football Club. 

Jana tarehe 30/03/2014 katika uwanja wa Ushirika Moshi ni siku ambayo timu ya Panone Fc na Machaa Fc zilishuka Dimbani kukamilisha Ligi daraja la Tatu Mkoa Kilimanjaro. 

Panone FC Maarufu kama Matajiri wa Kutupwa, imeshiriki katika ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Kilimanjaro iliyokamilika jana kwa mchezo mkali uliochezwa kati ya Panone FC. Na Machava FC. Ambao mchezo huo umeisha kwa Panone FC kuwatandika Machava FC bao moja kwa mduara. Machava walifungwa mdomo mnamo dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza na mchezaji wa Panone FC, Tony Kingundu alipoipatia timu yake bao la pekee ambalo liliipa timu yake ushindi na mpaka mpira unamalizika bao hilo halikuweza kuongezwa wala kurudishwa. Ubingwa walioupata Panone FC utawapa nafasi ya kwenda kuwakilisha mkoa Kilimanjaro kwenye mabingwa wa mkoa.

Mchezo huo ulitawaliwa na kadi za njano tano ambazo nne walipewa wachezaji wa Machava FC ambao ni Gipson Pajo ambaye alikuwa ni golikipa, Mohamed Boss, Mrisho Mindu na Hassan Sembi, na kadi moja ya njano alipewa mchezaji wa Panone FC. 

Kwa upande wa Kocha wa Machava Fc, Abdalah Hussein aliwasifia wachezaji  na alipoulizwa kuhusiana na timu yake kuambulia kipigo hakukosa cha kujitetea alisema haya. “Wachezaji wa timu zote mbili wamecheza vizuri ila sikuridhishwa na waamuzi walikua wakipendelea upande mmoja”
Na kocha wa Panone FC, Atuga Manyundo yeye amejisifu na kusema “Mimi niliiandaa timu yangu vizuri na nilijiandaa kupata ushindi maana wachezaji wangu wapo kambini na wanafanya mazoezi asubuhi na jioni na pia watu hawataki mapinduzi katika mchezo wa mpira hapa Kilimanjaro na sisi tumekuja kufanya mapinduzi na tunataka Panone FC ifike ligi kuu” 

Na kwa ushindi huu wa Panone FC,  wataenda kukutana na timu za mikoa ya kanda ya kaskazini mwa Tanzania ambayo ni Tanga, Arusha na Manyara na kukamiliza jumla ya mikoa mnne. Ubingwa huo wa Panone FC. Umepatikana baada ya kufanikiwa kupenyeza kwenye timu 17 za mkoa wa Kilimanjaro zilizoshiriki katika kinyang’anyiro hicho cha kumsaka bingwa wa mkoa. 

Hata hivyo timu hizo 17 zilichujwa na kubaki timu 10 ambapo ziligawanywa katika makundi mawili yaliyokuwa na timu tano kwa kila kundi na baadae ukapita tena mchujo ambao ulizipunguza timu nne na kubaki timu sita kati ya kumi za awali, ambapo timu hizo sita zilicheza ligi na hatimaye Panone FC kuibuka mshindi, huku Afro boys ikishikilia nafasi ya pili na New generation kushika nafasi ya tatu.


No comments:

Post a Comment