Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, March 9, 2014

TIMU YA PAONE FC YAZIDI KUNYANYASA KATIKA LIGI MKOA KILIMANJARO...,

Timu inayokuja kwa kasi ndani ya Mkoa kilimanjaro Panone Fc inayomilikiwa na na kampuni ya Uuzaji na Usambazaji wa mafuta ya Panone and Co. Ltd imeweza kuendeelea kutoa kipigo baada ya Kuilaza Machava Fc kwa Goli moja kwa Sifuri katika mchezo uliorudiwa siku ya Alhamisi baada ya Mvua kunyesha siku ya Jumatano na kusababisha muamuzi wa mchezo huo kuhairisha mchezo uliorudiwa Alhamisi ndipo Timu ya Panone Fc ilipoitundika Timu hiyo kongwe mkoani Kilimanjaro ya Machava Fc. 
Katika kuonesha kuwa wamedhamiria kutembeza kipigo, Timu ya Panone Fc leo wameisulubu Timu ya Agip Kahe kwa magoli mawili huku Agip Fc wakiambulia Patupu.

 Mashabiki wa Panone Fc wakishangilia bila kuchoka wakati timu hiyo ikiwa uwanjani.

Katika mchezo huo uliopigwa leo mnamo wa saa kumi alaasiri Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote mbili zikionesha ushindani wa hali ya juu mpaka ilipofikia dakika ya 43 ndipo mshambuliaji wa Panone Fc alipoifumania nyavu na kuandika Goli la kwanza. Mpaka kufika mapumziko Panone Fc ilikua ikiongoza kwa goli moja. Katika kipindi cha pili mchezo ulikua wa kasi na wa kushambuliana mpaka dakika ya 67 Ben Rafael aliweza kuipatia Timu yake ya Panone Goli la Pili lililokamilisha furaha ya Timu yake na kuondoka na Ushindi mnono kwani mpaka mpiraunakwisha Panone Fc wameongoza kwa goli mbili huku wapinzani wao Agip Kahe wakiwa hawajapata kitu.

Meneja wa Kampuni ya Panone and Co. Ltd ndugu Gido Marandu Akizungumza na Wachezaji wakati wa mapumziko alipokwenda kushuhudia mchezo huo leo.

Huu ni mzunguko wa pili na wa lala salama kwa Ligi na Panone Fc wakiwa wanaongoza kwa Point sita mkononi huku wakiwa wakifuatiwa na timu ya  Generation Fc.

 "Tumeanza na Mungu Tunamaliza na Mungu" Kama wanasema wachezaji wa Panone Fc wakisali baada ya Mchezo.

No comments:

Post a Comment