Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, May 20, 2014

Askofu wa Kanisa La Victoria Atunukiwa Shahada Ya Udaktari

MOSHI viongozi wengi wa barani Africa wameshindwa  kuleta maendeleo katika maeneo wanayo yaongoza ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwawezesha wananchi wake kutokana na baadhi ya viongozi hao kuweka maslahi yao mbele na kuwasahau wananchi wao.

Hayo yamebainishwa na Meya
wa Mji wa Moshi, Jafari Michael, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Boma Mbuzi (Chadema), wakati akizungumza katika hafla ya kumtunukia Shahada  ya udaktari ya huduma, Askofu wa  kanisa la victorious, Sixbert Paul Mkeremi, sherehe hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu kutoka katika mataifa mbalimbali.

Alisema nchi nyingi za kiafrika zimekuwa zikiendelea kuwa chini kiuchumi kutoakana na viongozi kujilimbikizia mali wakiamini kuwa wao wanapaswa kuwa nazo na kusahau kuwa hata wananchi nao wanatakiwa kunufaika na rasilimali hizo.

Alisema uadilifu kwa viongozi wa Afrika zimesabaisha wananchi wengi kuendelea kuwa nyuma kimaendeleo na kuwataka viongozi hao kuwa na hofu ya Mungu ili kuweza kuzisaidia jamii katika kuwaletewa maendeleo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa chuo cha Afrika Graduate, ambacho kipo nchini Sierra Leone, Dkt Timothy Kazembe, alisema chuo hicho kimewekeza katika elimu ili kuweza kuisaidia jamii.

Dkt Kazembe alisema chuo hicho kimekuwa kikizalisha Maaskofu na wachungaji wenye elimu ambao watakwenda kutoa huduma za kiroho katika jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake Askofu Dkt Sixbert Paul Mkeremi, mbali na kushukuru kutunikiwa nishani hiyo ya udaktari, pia amewataka viongozi wenzake kusimama katika nafasi zao za kumtumikia Mungu.

Mbali na Sixbert mkeremi kutunukiwa shahada hiyo pia mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili hapa nchini Rose Mhando naye alitunukiwa Stashada na cheti cha kutambua mchango wake katika kueneza injili kupitia nyimbo.

No comments:

Post a Comment