Kanisa la KKKT dayosisi ya kaskazini kwa kushirikiana na shirika
la kimataifa la misaada kwa nchi za Afrika, NCA lenye makao yake makuu nchini Norway ,wameanzisha jumla ya vikundi vya
wajasiriamali 120 mkoani Kilimanjaro kwa
lengo la kuwajengea uwezo wa kiuchumi ili waondokane na umaskini .
Akiongea
wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa
vikundi hivyo, yaliyofanyika wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, katibu
mkuu wa
dayosisi hiyo Bw. Julius Mosi amesema >> "vikundi hivyo vilianza
kuandikishwa mwaka 2008 ,hadi sasa vina mtaji wa zaidi ya pesa za kitanzania milioni
250 zikiwa
ni fedha ambazo wanachama wamechangishana wao wenyewe."
Bw. Mosi amesema, >> "vikundi hivyo vimeanzishwa bila kuwa na
itikadi za kidini wala za kisiasa na kwamba tangu kuanzishwa kwa mpango huo
jamii imenufaika katika maswala mbalimbali ya kiuchumi hali ambayo imewawezesha
kuondokana na umaskini na kuishi maisha yaliyo bora ukilinganisha na maisha yao ya awali".
Mchungaji Andrew
Munisi ni mratibu wa vikundi hivyo ambapo amesema kupitia mpango huo vikundi
hivyo vinapatiwa semina mbalimbali zikiwamo za kuhusu utawala bora na utunzaji
wa mazingira ambapo wanapokutana kila wiki wanapanda miti katika maeneo maalumu.
Akifunga mafunzo hayo kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Hai Bw.
Edward Ntakiliho, amewataka wanasemina hao kuwa mabalozi wazuri, katika
kuieneza elimu waliyoipata kwa wenzao pia kuwa makini kwa kutoa taarifa kunako
husika pindi wanapobaini hujuma, ama kasoro katika vikundi vyao.
No comments:
Post a Comment