Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Sunday, May 25, 2014

Timu ya waTanzania waishio DMV yatoka na ushindi wa bao 5-0 dhidhi ya timu ya waTanzania waishio Mjini NYC

Katika Sikuku ya Memorial day inayoendelea nchini U.S.A waTanzania waishio nchini Washington DC na New York City wakutana katika burudani za mchezo wa  mpira wamiguu uliofanyika siku ya Jumamosi Mei 24, katika uwanja wa Walker Mills Park uliopo Mills Rd, Capitol Heights Mjini Maryland.
Mgeni rasmi katika burudani hiyo alikuwa Ofisa wa ubalizi wa Tanzania Nchini Marekani na Nexico Bwna Suleiman Saleh, akikagua vikosi vya timu zote mbili.
Kikosi kamili cha Timu ya waTanzania waishio New York City Nchini Marekani 
Katika burudani hiyo mchezo ulipangwa takriban mwenzi mmoja uliopita na kutangazwa katika blog ya blog VIJIMAMBO kuhusu burudani hiyo iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu na timu zote mbili ambazo zilikutana na kuminyana vikali na hatimae Timu ya waTanzania waishio New York City kushindwa kutawala mchezo huo  kwa kufungwa bao 5-0  dhidi ya timu ya waTanzania waishio Washington D.C
Katika mchezo huo uliojaa burudani ya aina yake Timu ya waTanzania New York City walionekana kutawaliwa katika kipindi cha kwanza huku wakionyesha umahiri wakutaka kupangoa ngome ya Washington D.C lakini waliwezwa kukatishwa tamaa mnamo dakika ya 35 kipindi cha kwanza pale mchezaji  machachari wa Timu ya waTanzania Washington D.C David Ndunguru alipoaza kupasua nyavu kwa kombora kali na kujikuta New York kusambaratizwa katika kipindi cha kwanza kwa kufungwa bao mbili bila zilizovungwa na forward ya DMV David Ndunguru mwenye ustadi wa kujaribu makombora ya mbali.
Kikosi kamili cha Timu ya waTanzania waishio Washington DCNchini Marekani
 Wachezaji wa Timu ya waTanzania Washington D.C wakilinda goli lao kwa umahiri huku nyanda wa timu hiyo Mussa Linga akiwa makini na mpira ulioelikea katika hima yake.
Kipindi cha pili Timu ya waTanzania Washington D.C iliingia na kasi za jabu baada  ya kufanya mabadiliko ya kuongeza nguvu  kwa kumuingiza mchezaji Abdul Riyami ambae alifunga bao za kuwakatisha tamaa ya timu New York kwa makombara ya hapa na pale kwa bao la tatu na la nne kwenye dakika za 65 na dakika 74 na kujikuta wapinzani wakiacha mdomo wazi katika dakika hizo.
Bao la tano lilifunwa  na mchezaji maarufu na mkongwe hapa Washington D.C   Dedie Rouba katika dakika ya 82 na kuwaacha timu hiyo kukata tamaa hadi pale refa alipopuliza penga ya mwisho huku Timu ya waTanzania waishio DMV kutoka na ushindi wa bao 5-0 dhidhi ya timu ya waTanzania wa New York. 


Credit: Abou Shatry Washington D.C

No comments:

Post a Comment