Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, May 17, 2014

Majengo Ya K.N.C.U Mkoani Kilimanjaro Yashikiliwa na CRDB Bank

Hili ni moja kati ya majengo yanayomilikiwa na K.N.C.U

MOSHI mali za Chama  kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro, KNCU yakiwemo majengo makubwa yenye thamani ya shilingi bilioni 15 yanashikiliwa na benki ya CRDB,  kutokana na malimbikizo ya madeni ya  mikopo amabayo hadi sasa yamefikia kiasi cha shilingi bilioni 3.2  ambayo inadaiwa chama hicho kilikopa kutoka CRDB Bank.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mwenyekiti wa  KNCU, Maynard Swai,  alisema >> "Mpango wa chama hicho wa kupunguza madeni hayo ulikuwa uendane sanjari na uuzwaji wa shamba  la Gararagua lenye
ukubwa la wa zaidi ya hekari 3,000 lililopo wilayani Siha mkoani hapa."


Maynard Swai alisema >> "Pamoja na serikali kukubali uuzwaji wa shamba hilo kupitia Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini, mapema wiki hii Serikali imezuia  uuzwaji wa shamba hilo."

Amesema kwa hivi sasa chama cha KNCU, kimekuwa kikilipa kiasi cha shilingi milioni 500, kila mwaka kwa lengo la kupunguza deni la kulipa riba, licha ya mapato ya chama hicho hayatoshi kumaliza deni hilo.

Aidha Swai aliongeza kuwa  kutokana na serikali kutokuwa na maamuzi sahihi na kuizuia KNCU kuuza shamba hilo, chama hicho kipo katika mchakato wa kujinasua na deni hilo, kwa kuanza na ulipaji wa madeni hayo.

No comments:

Post a Comment