Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, May 17, 2014

UTATA WATANDA CHUO CHA SMMUCo KATIKA MCHAKATO WA KUMTAFUTA RAISI MWAKA 2014/2015

Pichani ni Renatus Hemed kushoto mgombea wa kiti cha uraisi ambaye inasemekana mpaka sasa ndio anaongoza kwa kura nyingi, akiwa na makamu wake.

Baadhi ya wanafunzi wakimshangilia mmoja wa wagombea uraisi ambae mpaka sasa ndio anaongoza kwa kura nyingi.


Shamra shamra za wanafunzi katika eneo la SMMUCo

MOSHI baada ya mchakato wa wagombe uraisi kunadi sera zao katika chuo kikuu cha SMMUCo chenya Campus kuu tatu ambazo ni Campus ya mjini, Campus ya Masoka pamoja na Campus ya Mwika, hatimaye wanafunzi wa SMMUCo wampata raisi atakaye waongoza kwa mwaka 2014 hadi 2015.

Mchakato huo ulianza jumatatu ya tarehe 13 mwezi wa May 2014, ambapo kila Campus za Campus ya mjini, Masoka Campus ziliweza kutoa mgombea mmoja mmoja katika kiti cha uraisi lakini kwa lakini Campus ya Mwika waliweza kutoa wagombea watatu wa kiti cha uraisi.

Mchakato mzima wa wagombea kunadi sera zao ulifanyika kwa siku tatu mfululizo mpaka siku ya ijumaa ya tarehe 16 ambayo ilikuwa ni siku ya wanafunzi wa SMMUCo walipata fursa ya kupiga kura. Kila Mwanafunzi aliweza kupiga kura katika Campus yake.

Mpaka inafika ijumaa usiku Renatus Hemed ambaye ni mgombea kutoka Campus ya Mjini alikua anaongza kwa kura nyingi katika kiti cha uraisi lakini mpaka sasa tume ya uchaguzi ya muda iliyochaguliwa chuoni hapo haijatoa matokeo rasmi na kumtangaza rasi wa SMMUCo kwa mwaka 2014/2015.

No comments:

Post a Comment