Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, May 27, 2014

Mfahamu Ras KENOO Kijana Wa Kitanzania Mwenye Vipaji Zaidi Ya Vitano.
Hii ni studio inayomilikiwa na Ras KENOO, pembeni yupo na Dj Virus

Dj Virus akiwa ameshika baadhi ya screen ambazo amezitengeneza Ras KENOOZote hizo hapo juu ni kazi alizofanya Ras KENOO.


Kenneth Tenga maarufu kama Ras KENOO ni mkazi wa majengo, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Ni mwanaharakati ambae anajitahidi sana kufanya harakati nyingi za kimaisha ili kujikwamua katika wimbi la umaskini.
Ras KENOO ana kundi lake linalofahamika kwa jina la Black Market Music lenye maskani yake mjini Moshi.
Na mpaka sasa tayari wana nyimbo takribani tatu ambazo zipo kwenye vituo mbalimbali vya radio na nyimbo zote hizo zimeandaliwa katika studio ya Ras KENOO ambayo ipo maeneo ya Majengo mjini Moshi.

Hizi ni baadhi ya kazi ambazo anafanya kwa sasa:-
  • Ni muandaaji wa muziki (Producer) wa muziki aina mbalimbali.
  • Ni muimbaji wa muziki wa Hip Hop.
  • Ni mbunifu (designer)  wa nembo au logo mbalimbali.
  • Anatengeneza screen kwa ajili ya kuweka nembo ana majina katika Tishirt mbalimbali.
  • Pia anauza plain tishirt zenye quality nzuri na kwa bei rahisi.
 Kwa yeyote anayeppenda kufanya kazi na Ras KENOO anaweza kumtafuta kwa namba hizi hapa +255658040792 Na yupo tayari kufanya kazi na mtu yeyote.

No comments:

Post a Comment