Oscar enzi za uhai wake.
MOSHI
kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Oscar John Njau mwenye umri wa miaka 24 ambaye
alikuwa ni dereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda, mkazi wa rau madukani, mjini
Moshi amefariki dunia baada ya kunywa
sumu. Tukio hilo la kustajabisha lilitokea jana tarehe 26 Mei 2014 majira ya saa
saba mchana.
Maelezo kutoka kwa ndugu
waliokuwa wanaishi nyumba moja na Oscar wanasema kuwa siku ya tukio Oscar aliamka asubui
na kujiandaa na kuelekea kwenye shuhuli zake za kuendesha bodaboda kama ilivyo kawaida yake. Lakini ilipofika majira ya saa nne abuhi,
Osca alirejea nyumbani na kuiegesha pikipiki yake kisha akawa anazunguka
zunguka eneo la nyumbani.
Baada ya muda kidogo alielekea nyuma ya choo ambapo
inadaiwa kuwa ndipo ilipokuwa imehifadhiwa sumu hiyo na kuichukua na kuamua kunywa na baada ya hapo alielekea
kwenye duka lililopo karibu na nyumbani kwao na kununua pombe inayohifadhiwa
kwenye mfuko mdogo maarufu kama kiroba na kuanza kunywa.
Baada
ya kunywa kiroba alianza kutapika na kwa watu waliokuwa hapo dukani wanasema alikuwa akitapika matapishi yaliyokuwa na harufu kali sana ya aina ya sumu aliyokuwa amekunywa, ndipo watu wale wakashtuka na kuamua kuwaita ndugu zake na Oscar. Ndugu zake walipofika walimuangalia Oscar na kutokana na hali aliyokuwa nayo wakawa na wasiwasi kuwa alikunywa sumu na walipo muuliza Oscar alikiri kuwa kweli amekunywa sumu.
Ndugu zake wakafanya juhudi za kumtapisha na baadae kuamua kumpeleka hospitali ya
rufaa ya Mawenzi, baada ya kufika hospitalini wauguzi walifanya jitihada za
kuokoa maisha ya Oscar kwa kumpa dawa na kumtapisha sumu lakini juhudi za
wauguzi hazikufanikiwa kwakuwa sumu ilisha sambaa mwilini kwa kiasi kikubwa sana. Na ilipofika
majira ya saa saba mchana Oscar alifariki.
Sababu
zilizompelekea Oscar kuamua kunywa sumu mpaka sasa hazijafahamika vizuri, japo kuna tetesi zisizo rasmi kuwa ni maneno yaliyokuwa yakiongelewa na mama yake wa kambo, na ni maneno ambayo hayakumfurahisha Oscar. Mtandao huu wa king Jofa bado unafuatilia ili kuweza kufahamu ukweli zaidi.
Na
taarifa kutoka kwa ndugu wa Oscar ni kwamba atazikwa siku ya ijumaa ya tarehe 30
Mei 2014.
Timu
nzima ya King Jofa inawapa pole ndugu, jamaa na marafiki wa Oscar John Njau.
No comments:
Post a Comment