MOSHI mfanyabiashara
mmoja ambae ni mkazi wa kijiji cha Kindi Msasani wilayani
Moshi mkoani Kilimanjaro amejiua kwa kujipiga risasi shingoni mara badaa ya
kuugua kwa muda mrefu.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Koka Moita alisema
tukio hilo lilitokea tareh 27 Mei 2014 majira ya saa 1:15 asubuhi katika kijiji cha Kindi Msasani.
Koka Moita
alisema kuwa mfanyabiashara huyo aliyefahamika
kwa jina la Wararimbo Lema mwenye umri wa miaka 74
alichukua uamuzi huo wa kujipiga risasi akiwa nyumbani kwake mara baada ya kuugua kwa muda mrefu. .
Moita alisema kuwa >> "Mfanyabiashara huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa ulioathiri mfumo wa koo pamoja na mfumo wa
chakula."
Kamanda huyo
alisema kwa sasa jeshi la polisi linaendela na uchunguzi ili kubaini ukweli juu
ya kifo cha mfanyabiashara huyo ili atua mbalimba za kisheria zeweze kuchuliwa.
Alisema mwili
wa marehemu umehifadhi katika hosptali ya rufaa ya KCMC kwaajili ya kuandaa
taratibu za mazishi ya mfanyabishara huyo.
No comments:
Post a Comment