Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, May 9, 2014

MWENYEKITI AWAHAMASISHA WANANCHI KULINDA VYANZO VYA MAJI KATIKA WILAYA YA SIHA

HAI inasemekana vitendo vya uharibifu wa vyanzo vya maji katika kitongoji cha Tindigani, kata ya Makiwaru wilayani Siha mkoani Kilimanjaro kama havitazibitiwa mapema huenda vikashindwa kuendelea kutoa maji kutokana na baadhi ya wakazi wa kitogoji hicho kuendesha shughuli za kilimo, ukataji wa miti hovyo, kujenga karibu na vyanzo hinyo vya maji, pamoja na kuchunga mifugo katika maeneo hayo.

Malalamiko hayo yametolewa na Mwenyekiti wa kijiji hicho anayefahamika kwa jina la Mussa Idd wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea vyanzo hivyo ambavyo ni kwa Njoke, na Noe Nasar na kujionea uharibifu mkubwa unao endelea kufanywa na wananchi wa maeneo hayo ndani ya mita takribani sitini ya nyanzo vya maji ambao ni kinyume na utaratibu.

Musa Idd alisema >> “hili suala inabidi tuangalie kwa kina zaidi, hapa wataalamu wanaosimamia mazingira tunao hatuelewi wanafanya kazi gani, tufute mambo ya siasa turudishe uoto wa asili katika vyanzo vyetu ili tuweze kuepukana na tatizo linaloweza kutokea hapo baadaye”

Pamoja na hayo pia aliwaomba wananchi kupanda miti kwa wingi ambapo alisema >> “katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha ni vyema wananchi wakapanda miti mbali mbali ikiwamo ya matunda ,pia alishukuru Shirika la Floresta kwa juhudi zao za kuelimisha jamii kuhusu mazingira”

Naye afisa mtendaji wa kata ya Makiwaru Issack Nasari alisema >> “itakuwa si busara kuongea kwa mzaha kuhusiana na suala hilo la vyanzo vya maji ni vyema ushirikiano ufanyike katika hili kwa kuhakikisha vyanzo hivyo vinalindwa kwa gharama yeyote,nina uhakika baada ya miaka kadhaa ijayo miji yetu itaingia kwenye tatizo kubwa la upatikanaji wa maji kutokana na vyanzo hivyo kuendelea kuharibiwa”

Aliendelea kusisitiza kuwa >> “elimu itolewe kwanza kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na suala lisiishie kuzungumzia kwenye vikao tuu”

Piaa aliwataka wananchi kuacha kutupa uchafu kwenye mto wa Biriri na akaema kutokana na soko la Makiwaru kutokuwa na sehemu ya kutupa takataka wakazi wengi wamekuwa wakitupa uchafu kwenye chanzo hicho jambo ambalo ni hatari kwa afya, na kuongeza kuwa wapo mbioni kutafuta eneo la kutupa taka kwa sasa.

No comments:

Post a Comment