Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, May 8, 2014

MWANAKE ANYONGWA NA CHANDARUA MPAKA KUFA KISHA KUTELEKEZWA KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI

Mwanamke mmoja mkazi wa Moshi mjini ameuwawa kikatili kwa kunyongwa kwa kamba ya chandarua, na mwili wake kuachwa uchi katika nyumba ya kulala wageni iliyopo mkoani Kilimanjaro maeneo ya Moshi mjini.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Kilimanjro Robert Boaz, alisema tukio hilo lilitokea mwezi Mei 6 mwaka 2014 majira ya saa 10:00 jioni katika nyumba ya kulala wageni iliyofahamika kwa jila la “Lomwe Gest House” iliyopo mjini Moshi.

Akizungumzia mazingira ya tukio hilo kamanda Robert Boaz alisema mwanamke huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja mwnamke huyo ambaye amekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati 24-26 alikutwa akiwa amenyongwa katika chumba alichokuwa akilala yeye na mwamaume mmoja anaye daiwa kuwa ni mpenzi wake.

Kamanda Robert Boaz alisema kuwa mwanamke huyo na mwenzi wake walifikia katika nyumba hiyo na waliishi kwa muda wa siku takribani tatu na kwamba mwanamke huyo alikuwa na tabia ya kutoka na kwenda kula na kisha kurudi na kwamba kwa siku hiyo hakutoka na ndipo wahudumu katika nyumba hiyo wakachukua hatua ya kuvunja mlango.

 Alisema mara baada ya kuvunja mlango huo walikuta mwili wa mwanamke huyo ukiwa kitandani uchi na umenyongwa kwa kamba ya chandarua huku nguo zake zikiwa pembeni ambapo mara baada ya tukio hilo mwanaume huyo alikimbia.

Aidha alisema mwanaume huyo alijiandikisha katika kitabu cha wageni kwa jina la Yusuph Hamisi na kwamba jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linaendelea kufanya uchunguzi kujua chanzo cha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kumtafuta muaji huyo.

Kamanda Robert Boaz alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hosptali ya rufaa ya KCMC na kuwataka wananchi waliopotelewa na ndugu zao kwenda kwaajili ya kuutambua mwili huo.

No comments:

Post a Comment