Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, May 10, 2014

TaCRI YAWAHAMASISHA WAKULIMA WA KAHAWA KUPANDA MICHE BORA AINA YA CHOTARA

MOSHI taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI), imesema ili kuleta mapinduzi ya kijani katika kilimo, hususani katika kilimo cha zao la kahawa, yawapasa wakulima hapa nchini kutumia miche bora aina ya chotara inayozalishwa na taasisi hiyo.

Hayo yamesemwa na mtaalamu wa usambazaji wa teknolojia na mafunzo
wa TaCRI, Jeremia Magesa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Jeremia Magesa alisema >> “kushuka kwa ubora wa zao la kahawa kumechangiwa kwa kiwango
kikubwa na wakulima wenyewe”  ambapo alishauri umuhimu wa kutumia miche ya chotara ambayo ni bora na yenye uwezo wa kukabiliana na magonjwa ya chulebuni na mnyauko fuzari.

Mtaalamu huyo aliwataka wakulima wa zao la kahawa, kufuata sharia na kanuni
bora za kilimo ili kuweza kujiletea mapinduzi ya kilimo na kwamba TaCRI katika kutatua matatizo ya uzalishaji, imefanikiwa kugundua aina mpya tatu chotara za miche ya kahawa aina ya Robusta

Jeremia Magesa alisema >> “Katika nchi za ulaya mapinduzi ya kijani, yameweza kufanikiwa kwa
kiasi kikubwa baada ya wakulima kufuata kanuni bora za kilimo hasa kilimo cha zao la kahawa”

Pia Jeremia Magesa aliongeza kuwa katika ugunduzi huo, TaCRI imefanikiwa
kugundua aina mpya 15 bora za miche chotara ya kahawa aina ya arabika huku akiwataka wakulima wa kahawa kuacha desturi ya kilimo cha mazoea ambacho hakikidhi mahitaji.

Aliongeza kwa kusema >> “Ili Taasisi iweze hii iweze kufikia malengo yake, na kuwawezesha
wakulima kuleta mapinduzi ya kijani, wakulima hawana budi kufuata maelekezo ya wataalamu, tuachane na kilimo cha mazoea, ifike muda wakulima wa kahawa tukubali kubadilika na kufuata ushauri tunaopewa,”

Hata hivyo Magesa aliziomba Halmashauri zote nchini, kushirikiana na
vyama vya msingi vya ushirika kwa kuwapa miche bora ya kahawa kama moja ya njia za kuongeza kiwango cha ubora cha uzalishaji wa kahawa nchini kama ilivyokuwa katika miaka ya 70.

Aisema >> “Sisi TaCRI sio wasambazaji wa mbegu za kahawa , tunasambaza
teknolojia na mafunzo kwa wakulima, ifike mahala Halmashauri zetu zione umuhimu wa kuwapa msaada wakulima na vyama vya msingi ili kuwawezesha kufikia malengo ya kufanya mabadiliko ya kijani,”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TaCRI, Profesa James Teri, akizungumzia
aina hiyo mpya ya miche alisema miche bora chotara za kahawa zimekuwa ni mkombozi mkubwa katika sekta ya kahawa kwa kuwa zina tija ya hali ya juu zaidi ya aina za zamani.

Profesa Teri alisema>> “ aina hizo za miche
 zina muonjo wa hali ya juu kama aina za zamani au hata zaidi na zina ukinzani na magojwa hatari ya chulebuni (CBD) na kutu ya majani (CLR) na kwamba  kutokana na sifa hizo, aina hizo mpya zinampunguzia mkulima gharama za uzalishaji, kati ya asilimia 30 na 50 ukilinganisha na miche mingi ya zamani ambayo mingi imezeeka”

No comments:

Post a Comment