Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Saturday, May 10, 2014

WATU WAWILI AMBAO NI MKE NA MUME WAUWAWA KIKATILI NA MTOTO WAO

MOSHI watu wawili wa familia moja ambao ni mke na mume wameuwawa kikatili na mtoto wao wa kiume kwa kuwakatakata na kitu kilichosadikika kinaweza kuwa ni panga hadi ubongo kumwagika na kupelekea mauti kuwafika baada ya muda mfupi. Tukio hilo la kustaajabisha limetokea wilayani Hai mkoani kilimanjaro.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz amewataja marehemu kuwa ni Shahidu Mohamed Njau, miaka 60, na Minayi Mohamed Peter, miaka 57, wote wakazi wa kijiji cha Roo Kata ya Masama Mashariki wilaya ya Hai.

Aliendelea kusema >> "Muuaji anajulikana kwa jina la Yusuph Shahidu Njau miaka 32 na taarifa za mwenyekiti wa serikali ya kijiji anasema tukio hilo lilitokea tarehe 9 mwezi May 2014 saa 12 jioni."

Kamanda Boaz alisema >> "Mara baada ya kijana huyo kufanya tukio hilo, alichoma moto nyumba ya wazazi wake hao ambayo walikuwa wakiishi, ambapo majirani walifanikiwa kuzima moto huo kabla ya kuleta madhara makubwa."

Boaz alisema >> "Chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba mtuhumiwa huyo mara baada ya kufanya tukio hilo alikimbia pasipo julikana."

Kamanda alisema >> "Jeshi la polisi, linaendela kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo pamoja na  kumsaaka mtuhumiwa ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake."

Miili  ya marehemu imehifadhiwa katika hosptali ya wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, ikisubiri  taratibu za mazishi.
 
Kwa upande wa mwenyekiti wa kijiji hicho Alfan Mohamed alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo na alisema >> "Baada ya kutoa msaada wa kuzima moto waliingia ndani na kumkuta mama ameshafariki na baba mzazi akiwa mahututi na alipoteza maisha akiwa njiani eneo la kwasadala akipelekwa hospitali."

No comments:

Post a Comment