Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, June 17, 2014

BILIONI MOJA KUTUMIKA KUJENGA BARABARA NA DARAJA KATIKA WILAYA YA HAI

SERIKALI imetenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwaajili ya ujenzi wa barabara za vijijini wilayani Hai sambamba na fedha za ujenzi wa daraja la Kiungi almaarufu kama daraja la mnepo ambalo limekuwa likisababisha vifo vya watu kwa miaka mingi.

Hayo yalibainishwa na Katibu wa chama cha mapinduzi CCM mkoani Kilimanjaro Steven Kazidi, wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mijongweni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Steven Kazidi alisema kuwa milioni 357 zimetolewa na serikali kwaajili ya ujenzi wa daraja la Kiungi na kwamba tathmini iliyofanywa na wataalamu ilionesha kuwa zaidi ya shilingi milioni 400 zitatumika katika ujenzi wa daraja hilo hadi kukamilika.

Aidha alisema milioni 43 zilizobaki halmashauri itapaswa kuchangia milioni 30 huku milioni 13 ikiwa ni michango ya wananchi katika mradi huo wa maendeleo.

Alisema kutokana na tatizo la miundombinu mibovu na isiyopitika ya barabara katika vijiji mbalimbali katika wilayani ya Hai serikali imeona ni vema kutenga fedha hizo kwaajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo.

Katika hatua nyingine Steven Kazidi aliwataka wananchi wa kijiji hicho kusimamia mradi huo kikamilifu ili kuzuia ubadhirifu ambao unaweza kufanywa na baadhi ya viongozi katika halamshauri hiyo na kurudisha jitihada za serikali nyuma.

Nao baadhi wananchi Angel Poul na Fadhili Abdala walisema daraja hilo limekuwa ni kero kubwa kwao na kwamba baadhi ya watu wamepoteza maisha kutokana kuangukia ndani ya maji wakati wakijaribu kuvuka .

Walisema kujengwa kwa daraja hilo litatoa fursa kwa wakazi wa maeneo yao kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato kwa ukakika ikiwa ni pamoja na kupata soko la mazao ambayo walikuwa wakishindwa kuuza kutokana na kukosa mahala pakuvukia.

No comments:

Post a Comment