Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Tuesday, June 17, 2014

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI AKEMEA VIKALI UNYANYASAJI

MOSHI serikali imeitaka jamii kukemea vikali vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikifanywa ndani ya jamii, vikiwemo vitendo vya uwabakaji , ukeketaji pamoja na kuwaozesha wasichana katika umri mdogo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Kasimu Majaliwa, wakati wa Ufunguzi wa kongamano la Watoto lililofanyika katika ukumbi wa chuo cha ufundi VETA kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Naibu waziri Majaliwa, alisema kuwa serikali haita sita kuwachukulia hatua kali dhidi ya wazazi ambao wamekuwa wakiwafanyia watoto vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kubakwa, na kuwataka wazazi na walezi kuhakikisha swala hilo hawalifumbii macho na kulitaka jeshi la polisi nchini kuhakikisha wanatokomeza tatizo hilo.

Amesema kuwa ni jukumu la kila mzazi au mlezi kuhakikisha mtoto analindwa na kupatiwa elimu iliyo bora kama ilivyo kwa watoto wengine, na kuacha tabia ya wazazi kuwapa elimu watoto wa kiume pekee kwani kwa kufanya hivyo huo nio unyanyasaji pia.

Hata hivyo Naibu waziri huyo, ameyahimiza mashirika ya Serikali na watu binafsi, kuhakikisha wanajikita kuwasaidia watoto, katika swala la elimu na kuacha kujikita katika siasa zisizo na maana yoyote kwa jamii.

No comments:

Post a Comment