MOSHI meneja
wa kituo cha damu salama kanda ya kaskazini Dr. Wilhelmuss Mauka, amesema kutokuwa na damu katika hospitali
ni urasimu wa wauguzi pamoja na njaa za
manesi kuwataka wagonjwa kulipia damu hiyo
huku damu hiyo ikitolewa bure.
Dr. Mauka
alisema hayo jana katika siku ya uchangiaji damu nchini, iliyofanyika
katika viwanja vya ofisi vya benki ya damu KCMC manispaa ya moshi mkoani Kilimanjaro.
Alisema wagonjwa
wanapotozwa fedha ili wawekewe damu ni kosa na kwamba damu iko nyingi na hutolewa
bure kama wananchi wanavyochangia.
“kulipia
damu kwenye mahospitali ni kosa damu inatolewa bure katika hospitali zote bila
kubagua ya serikali na binafsi wanachokifanya wauguzi kutoza wagonjwa damu hiyo
ni kosa na ni urasimu tu unakuwapo katika hospitali husika." alisema Mauka.
Dr. Mauka
alisema damu katika kituo hicho ipo yakutosha na kwamba kituo hicho hakijawahi
kupungukiwa na damu, na kwamba kila mwaka huwa wanavuka malengo ya ukusanyaji
wa damu kwa asilimia mia moja.
Kwa upande
wake mgeni rasmi ambaye ni Daktari wa chuo cha polisi moshi Francis Ngozi, alisema
wamekuwa wakihamasisha polisi kuchangia damu
ili kuokoa maisha ya watu haswa wale wanapoata ajali za barabarani.
Dr. Ngozi alisema kutokana na kuwapo na ajali nyingi za
barabarani haswa zaitokanazo na bodaboda
ni vyema jamii ikajitokeza kuchangia damu ili kuweza kuokoa maisha ya
wananchi.
No comments:
Post a Comment