Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, June 13, 2014

Shirika La NSSF Latoa Msaada Wa Sare Za Shule Kwa Wanafunzi 25 Yatima Na Wale Wasiojiweza

MOSHI shirika la Mfuko wa Taifa  wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoani Kilimanjaro limetoa sare za shule kwa wanafunzi 25  yatima na wanaoishi katika mazingira mgumu, wanafunzi hao wanaosoma katika shule ya msingi Mwenge iliyopo manispaa ya moshi.

Akikabidhi sare hizo kaimu meneja wa NSSF mkoani Kilimanjaro  Albert  Kibonde, alisema >> "Shirika hilo limekuwa likitoa msaada kwa watu wenye uhitaji hasa wale wanaoishi katika mazinga magumu na hatarishi."

Kibonde alisema mchango wa huo umetoka kwa wafanyakazi wa NSSF na kwamba kila mwaka wanatoa mchango kwa jamii yenye mahitaji na wasiojiweza, pamoja na wale wenye mahitaji muhimu.

“Sisi kama wafanyakazi wa NSSF huwa tunachanga fedha kwa ajili  ya kusaidia watu ambao hawana  uwezo na tumeona kwa awamu hii tuwapatie sare watoto ambao wanaishi katika mazingira magumu” alisema  Kibonde

Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi mwenge Pasfia Ernest, alishukuru shirika NSSF kwa kusaidia watoto hao sare za shule  na kwamba wanafunzi hao wametoka katika familia duni ambazo zinashindwa kuchangia chochote.

Ernest  alisema shule hiyo ina jumla ya  watoto 25 ambao hawana uwezo na kwamba hata madaftari huwa wananunuliwa na shule hiyo.

“Watoto hawa huwa wanalele  na bibi na wengine na majirani  na watu ambao wanaishi na watoto hawa nao hawana uwezo mara nyingi shule ndio inayowatimizia mahitaji yao ya shule kwa kutumia faida inayopatikana katika duka la shule” alisema mkuu huyo.

No comments:

Post a Comment