Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, June 18, 2014

HUU NDIO UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2014

54,085 wachaguliwakati ya 71,527 waliostahili.

Ofisi ya waziri mkuu, tawala za mikoa na serikali za mitaa - TAMISEMI imetangaza wanafunzi waliochaguliwa kuingia kidato cha tano mwaka 2014, katika jumla ya shule 241 zikiwemo shule 33 ambazo ni mpya pamoja na vyuo vya ufundi kulingana na takwimu za matokeo ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2013.

Akitangaza uchaguzi huo jijini dar es salaam naibu waziri wa elimu - TAMISEMI, Bwana Majaliwa Kassim Majaliwa amesema jumla ya watahiniwa 427,679 walisajiliwa kufanya mtihani huo kati ya hao watahiniwa 404,083 sawa na asilimia 94.48 walifanya mtihani na watahiniwa 23,596 hawakufanya mtihani.

Bw. Majaliwa amebainisha kuwa jumla ya wanafunzi 54,085 sawa na asilimia 75.61 ya wanafunzi 71,527 waliostahili kuingia kidato cha tano tanzania bara wamechaguliwa huku jumla ya wanafunzi 16,800 wakiwemo watahiniwa 10 wa kujitegemea wakikosa sifa za msingi za kuchaguliwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ufinyu wa nafasi za kidato cha tano na sita na kukosa tahasusi (combination) ambao baadhi yao watapata nafasi katika uchaguzi wa awamu ya pili.

Katika kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu katika mtihani huo wanaendelea na masomo serikali imeweka utaratibu wa kuwapatia nafasi ya kusoma kidato cha tano na cha sita kwa pamoja na shahada ya ualimu wanafunzi wenye sifa.

Kwa mujibu wa naibu waziri Majaliwa, wanafunzi wote waliochaguliwa wametakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa julai 10 mwaka huu 2014  na wale ambao watashindwa kuripoti hadi kufikia julai 30 bila taarifa nafasi zao zitajazwa na wanafunzi waliokosa nafasi.

No comments:

Post a Comment