SIHA jeshi la Polisi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro limewatahadharisha wananchi wote hasa
mashabiki wa mpira wa miguu maarufu kama soka kuwa makini na vitendo vya uhalifu vinavyaweza
kujitokeza katika wakati huu wa fainali za michezo ya kombe la Dunia
lililoanza tarehe 12 Juni 2014 huko nchini Brazili.
Tahadhari
hiyo imetolewa leo na mkuu wa Polisi Wilaya ya Siha [OCD] Lutusyo Mwakyusa
wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu usalama
wa raia na mali zao kutokana na kuanza kwa michuanao
ya kombe la Dunia ambapo kwa kiasi kikumbwa michezo hiyo hufanyika
nyakati za usiku
Mwakyusa
alisema kufuatia kuanza kwa kombe la dunia na kutambua kwamba michuano
hiyo inatazamwa na watu wengi katika maeneo mbali mbali kupitia Luninga
Jeshi hilo linatoa tahadhari kwa wananchi wote hasa mashabiki wa michezo
hiyo kuwa makini na vitendo vya kihalifu vinavyoweza kujitokeza katika
kipindi hicho
Aidha
aliwataka wamiliki wa Kumbi mbalimbali, Bar na sehemu mbali mbali zinazotumika
kuonesha michuano hiyo wametakiwa kuzingatia uhalali wa vibali vyao
ikiwamo kuwa makini na vitendo vyovyote vitakavyo ashiria uhalifu na
kutoa taarifa kwa vyombo usika
Mbali
na kutoa taarifa za uhalifu pia wametakiwa kuzingatia hali ya usalama
ndani ya ukumbi kwa kuweka madirisha makumbwa ili watazamaji waweze
kupata hewa safi ili isije tokea kama ilivyotokea huko Tabora miaka ya
hivi karibu ambapo watu kadhaa waliumia kutokana na msongamano mkubwa wa watu.
Pia
Wananchi wote wanapaswa kuwa makini na mali zao wakati wote wa michuano
hiyo kwa kuweka ulinzi katika makazi yao kuimarisha falsafa ya ulinzi
shirikishi inayoimiza kutoa taarifa pindi unapoona kiashiria chochote
cha uhalifu iwe nyumbani kwako au kwa jirani yako.
No comments:
Post a Comment