Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, June 16, 2014

MILIONI MIA TISA ZILIZOPATIKANA MLIMANI KILIMANJARO KUSAIDIA WATU WENYE VVU/UKIMWI

Ally Buruan akiwa na wageni.

KILIMANJARO serikali imesema itaendelea kushirikiana na wadau wa utalii zikiwemo taasisi na makampuni mbalimbali katika kuhakikisha kuwa inaimarisha miundombinu katika mlima Kilimanjaro ili kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wageni pia kuimarisha sekta ya utalii ambayo inachangia uchumi kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu wakati akizindua ziara ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa wafanyakazi wa kampuni ya madini ya Geita (GGM) uliofanyika kwenye lango la machame wilayani Hai mkoani Kilimanjao.

Meneja wa mawasiliano wa GGM Bwana Tenge Tenga amesema ziara hiyo iliyokuwa na lengo la kuhamasisha jamii kupanda mlima Kilimanjaro, pia kupata fedha zitakazotumika kusaidi jamii katika kukabiliana na VVU na ukimwi, ambapo kwa mwaka huu wamekusanya milioni mia tisa (900,000,000)  nakuiomba jamii na taasisi mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo.

Mkurugenzi wa tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt.  Fatma Mrisho amesema mapato yanayo tokana na wa wageni wanaopanda katika mlima Kilimanjaro yanachangia kwa kiasi kikubwa shughuli mbalimbli za kimaendeleo pia imepunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi ya VVU na UKIMWI hapa nchini Tanzania.

Akiongea kwa niaba ya mkurugenzi mkuu mkuu hifadhi ya taifa Tanzania TANAPA, mkurugenzi mkuu wa mipango TANAPA Bw. Ezekil Dembe alisema mlima Kilimanjaro unamanufaa makubwa si kwa Tanzania peke yake bali ni kwa dunia nzima hivyo kila mmoja anawajibu wa kuulinda na kuutunza mlima Kilimanajro.

No comments:

Post a Comment