Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, June 25, 2014

MABWANA SHAMBA WATAKIWA KUWATEMBELEA WAKULIMA MASHAMBANI

HANDENI Mabwana shamba wilayani Handeni nkoani Tanga wametakiwa kuwatembelea mara kwa mara wakulima katika mashamba yao badala ya kukaa tu ofisini na kutoa maelekezo kwa wakulima bila kujua mazingira ya shamba kama ni sawa na maelekezo wanayotoa.

 Katibu tawala wa wilaya ya Handeni, John Ticky Alisema hayo juzi alipotembelea mashamba darasa ya wakulima wa vijiji vya Magamba na Kwabaya katika kuadhimisha siku ya mkulima kiwilaya ambapo wilaya imejipangia utaratibu wa kuwa na siku ya wakulima kiwilaya.

Alisema kuwa ni vizuri maafisa wa kilimo kujenga tabia ya kutembelea shamba la mkulima ili wakati akitoa ushauri ajue mazingira halisi ya shamba kwani inawezekana halihitaji mbolea ila mkulima akashuriwa atumia mbolea kitu ambacho sio sahihi.

Ticky alisema endapo mkulima atafundishwa kanuni zote za kulima kilimo bora kwa kufuata kalenda ya kilimo, mbolea na mbegu bora lazima  na afisa kilimo baadae lazima mavuno yatakuja yakutosha ambapo ataweza kuuza ili kujikimu kimaisha na kuweka akiba kwaajili ya msimu mwingine unaofuata.

Maafisa kilimo lazima wajenge tabia ya kutembelea mashamba ya wakulima wao mara kwa mara badala ya kutoa  ushauri wa mezani ambao unaweza kumrudisha nyuma mkulima kwani anaweza kutumia ushauri ambao sio sahihi kutokana na mazingira ya shamba jinsi yalivyo” alisema Ticky

Pia aliongeza kwasasa halmashauri tayari imeshaongeza matrekta hivyo kila  kata wilayani Handeni lipo kwaajili yao kitu muhimu ni mkulima kusafisha shamba lake mapema na kuondoa visiki halafu watumie matrekta  hayo katika kilimo badala ya kutumia jembe la mkono peke yake.

Alimaliza ziara yake kwa kuwaasa wakulima kuacha tabia ya kuuza mazao yakiwa shambani kwa kudanganywa na wachuuzi ambao huwalalia kwa kuwauzia kwa bei ndogo na badala yake amewataka kuvuna na kuhifadhi mazao yao hadi pale chakula kitakapopanda bei ambapo na wakulima watauza kwa faida.

No comments:

Post a Comment