Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Monday, June 16, 2014

MTOTO WA AFRICA - HAI YAZINDUA KITUO CHA HUDUMA CHA KUSAIDIA WANAWAKE NA WATOTO

Juni 16 ya kila mwaka Umoja wa Afrika sambamba na washirika wake husherekea siku ya mtoto wa Afrika au kwa lugha ya kiingereza “Day of African Child (DAC ),”  ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka 1976 ambapo waandamanaji wanafunzi wa shule za Soweto Afrika ya Kusini waliandamana kupinga elimu iliyokuwa inatolewa kwa manufaa ya utawala wa kibaguzi wa makaburu. Maandamano hayo yalipokelewa na mikono usio na huruma na masikio yasiyo sikivu ya utawala wa kibaguzi na kusababisha vifo vya mamia ya wanafunzi.

Mwaka 1991 Baraza Kuu la Umoja wa Afrika lilipitisha azimio na kuifanya Juni 16 ya kila mwaka kuwa ni siku ya kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika. Siku hii inatoa nafasi kwa wadau wote wa haki za watoto, zikiwamo serikali mbalimbali, mashirika yasiyo ya kiserikali na ata jumuiya za kimataifa kuyatazama kwa kina matatizo yote yanayowakabili watoto katika bara letu la Afrika.

Kwa mwaka huu yaani 2014 Umoja wa Afrika umetaja lengo Kuu la Siku hii ni kuzitaka serikali zote barani humu kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha watoto wanapata haki ya kupata elimu bora kulingana na mikataba mbalimbali juu ya haki za mtoto ya kimataifa inayosema. Pakiwa na kauli mbiu, ”KUPATA ELIMU BORA NA ISIYO NA VIKWAZO NI HAKI YA KILA MTOTO”

Katika kusherekea siku ya mtoto wa Afrika 16 juni 2014 Halmashauri ya Wilya ya Hai, ikishirikiana na viongozi wa Serikali, UNICEF na Save the Children imezindua kituo cha Huduma Jumuisho kitakachowasaidia Wanawake na Watoto ambao wameathirika na ukatili.

Katika kituo hicho huduma za kuwasaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ikiwa ni pamoja na huduma za afya, msaada wa kisaikolojia, ulinzi usalama na msaada wa kisheria vinaweza kutolewa hapo katika eneo moja ndani ya kituo cha afya zikiwa zimekarabatiwa vizuri zaidi alisema Cherles Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya afya na ustawi wa jamii.

Pollangyo alisema kua kituo hicho kitasaidia kupunguza madhara zaidi ya ukatili kwa sababu wahanga wa ukatili wataweza kupata huduma zote muhimu katika eneo moja na hawatakuwa na sababu ya kurudiarudia kuwaeleza watoa huduma mbalimbali walio katika maeneo tofauti yale mambo mabaya waliyoyapitia au kutakiwa kwenda na kurudi kutokana na kukosa wa uratibu na uwezo wa watendaji wa sekta mbalimbali.

Nae mwakilishi wa UNICEF Tanzania Dk, Jama Gulaid alisema kuwa kama tutafanya kazi kwa ushirikiano na Serikali na wadau wengine tunaweza kupata suluhu katika kumaliza ukatili dhidi ya watoto ukatili dhidi ya watoto uko kila mahali na hatuwezi kuendelea kuufumbia macho Watoto wote hapa tanzania wanahaki ya kuishi na kukua katika mazingira yasiyo na ukatili kama sisi sote tukifanya kazi kwa kushirikiana pamoja sina shaka tunaweza kumaliza ukatili dhidi ya watoto alisema.

No comments:

Post a Comment