Kamanda Boaz akiwa ameshikilia silaha ambazo zinaaminika zilikuwa zikitumika kwenye matukio ya ujambazi.
Watu wawili waaoshukiwa kuwa ni majambazi wamekatwa na
jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro wakiwa na bunduki mbili aina ya short gun
zikiwa zimekatwa mtutu ambazo zinakisiwa kuwa ndizozilizokuwa zikitumika katika
matuio mbalimbal ya kiuhalifu katika mkoa wa Kilimanjaro.
Akidhibitisha
kukamatwa kwa majambazi hao kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz
amesema kukamatwa kwao kunatokana na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kuanza
msako mkali, baada ya kuongezeka kwa matukio ya uhalifu ukiwemo wa kutumia ya
silaha.
Kamanda
Boazi amewataja watuhumiwa hao ni Ibrahimu Machaku mkazi wa kijiji cha kahe
wilayani Moshi aliye kamatwa na silaha ambayo inasadikiwa kuibwa katika chama
cha ushirika cha legomulo wilayani Moshi, pia wamemkamata Laurenti Massawe
mkazi wa jiji la Arusha alipovamia na kuiba nyumbani kwa mfanyabiasha mmoja Bw
Mehboo Sadik eneo la shant town mjini moshi akiwa na bunduki aina ya short gun
iliyokatwa mtutu.
Aidha
kamanda Boaz ameseama jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata madawa
yanayosadikiwa kuwa ni ya kulevya aina ya cocan ambayo yalikuwa yametelekezwa
ndani ya ndege ya Ethiopia air line katika kiwanja cha KIA kilichopo mkoani
Kilimanjaro na kwamba jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wakumpata muhusika wa
madawa hayo.
No comments:
Post a Comment