WATU watano wakiwemo wanawake wawili wamefikishwa katika
mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za
kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 16.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka katika kesi hiyo Beatus
John, washtakiwa hao, Charles Atanadi Kiule, January Alaji, Patrick Sapisi, Khadija
Salum na Namwaka Mbwana, wanadaiwa kutenda kosa hilo mwezi Novemba, mwaka jana (2013),
eneo la Lembeni, wilaya ya Mwanga, ambapo walimlawiti kijana huyo ambae jina
lake linahifadhiwa.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo, katika shtaka la
kwanza, washtakiwa Charles Atanadi Kiule, January Alaji na Patrick Sapisi, kwa
pamoja walimlawiti kijana huyo kwa zamu.
Aidha alisema katika shtaka la pili, watuhumiwa hao wawili
wanashtakiwa kwa kumjeruhi kijana huyo kwa kumchapa kwa fimbo na nyaya na
kusababishia maumivu makali na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huyo watuhumiwa Khadija
Salum na Namwaka Mbwana, wanakabiliwa na shtaka moja tu la kushawishi washtakiwa
wa kwanza hadi wa watatu kumbaka kijana huyo kwa madai kuwa alitaka kumbaka
mtoto wa mshtakiwa wa nne, Khadija Salum.
Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Emmanuel Gasper, aliiambia
mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao wana kesi ya kujibu ambapo aliihairisha kesi hiyo hadi Julai 2, mwaka huu.
Aidha wastakiwa namba nne na namba tano wanatarajiwa kutetewa
Rehema Mtuli kutoka jijini Dar es salam
huku wastakiwa namba moja hadi tatu hawana wakili wa kuwatetea.
upande wa mashtaka unatarijiwa kuleta mashahidi nane. Washtakiwa wote wako
nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment