WATU
watatu wamefariki dunia mkoani Kilimanjaro katika matukio matatu
tofauti, likiwemo tukio la mtu mmoja kujiua kwa kujinyonga na chandarua
cha kuzuia mbu akiwa chumbani kwake.
Akithibitisha
kutokea kwa matukio hayo Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Koka
Moita alisema tukio la kwanza lilitokea Juni 1, mwaka kuu, majira ya saa 8:00 mchana katika kijiji cha Kilema, Moshi Vjijini, mkoani Kilimanjaro.
Akielezea
mazingira ya tukio hilo kamanda Moita alisema Martin Michael, (45)
alikutwa akiwa amening’inia kwenye paa la chumbani kwake akiwa
amejinyonga kwa kutumia chandarua cha kuzuia mbu kilichokuwa
kimetundikwa kwenye kitanda alichokuwa akikitumia kulala.
Aidha
kamanda huyo alisema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana na kwamba
jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli
kuhusu chanzo cha tukio hilo na kwamba mwili wa marehemu huyo
umehifadhiwa katika chumba cha maiti kilichopo katika hosptali ya
Kilema.
Kamanda
Moita alisema katika tukio la pili mwanamke mmoja aliemtaja kama
Namkondo Hassani, (35) mkazi wa kijiji cha Msufini Kata ya Ndungu,
wilayani Same, alikutwa amekufa katika mfereji wa unaotumika kwa
umwagiliaji katika kilimo.
Aidha
kamanda huyo alisema katika tukio la tatu Juni 1, mwaka huu, mtu mmoja
aliemtaja kama Devotha Deusi, (24), alikutwa amekutwa amefariki dunia
nyumbani kwake eneo la Mdawi, Old Moshi.
Kamanda
Moita alisema kuwa maiti ya mwanamke huyo ilikutwa majira ya saa saba
za mchana wa siku hiyo na kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha ya kuwa
alifariki kutokana na ugonjwa uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment