MOSHI idadi ya wagonjwa wenye homa ya dengue, katika Manispaa
ya Moshi imeongezeka na kufikia wagonjwa watano, huku wengine 11 wamegundulika
kuwa na ugonjwa huo.
Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya
Manispaa ya Moshi, Dkt Christopha Mtamakaya wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake .
Dkt. Mtamakaya amesema wagonjwa watatu wamelazwa katika
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mawenzi, huku
wengine wawili wakiwa katika hospitali ya Jaffari, na wagonjwa 11 waliogundulika kuwa na dalili
hizo uchukuaji wa sampuli za damu unaendelea kufanyika katika hospitali hiyo.
Hata hivyo Dkt mtamakaya ametoa rai kwa wananchi kuacha
kutumia dawa bila kupima, pindi wanapojihisi kuumwa, na kwamba juhudi
zinaendelea kuchukuliwa na wataalamu wa afya ili kudhibiti ugonjwa huo kwa kuua
mazalia ya mbu.
Aidha Dkt Mtamakaya amewaomba wananchi waendelee
kufanya usafi wa mazingira, kufukia madimbwi na maji machafu pia kutumia
chandarua na kufika hospitalini pindi wanapoona dalili za kuumwa.
No comments:
Post a Comment