Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 17, 2014

WATATU WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA MIADARATI

MOSHI watu watatu wanashikiliwa Jeshi la polisi mkoani kilimanjaro, kwa tuhuma za kukamatwa na  kilo 150 pamoja na magunia 9 ya bangi yaliyokuwa yakisafirishwa kwenda  Tanga na nchi jirani ya Kenya.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,  Robert Boaz, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lilitokea julai 16 mwaka huu majira ya saa 6:00  mchana na kwamba magunia 9 yalikamatwa same mjini yakiwa yanapelekwa mkoani Tanga yakitokea jijini Arusha.

Kamanda alisema askari wa doria walikamata magunia hayo yakiwa yamepakiwa kwenye gari alina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T879 CCU, ikiwa imepakia kiasi hicho cha bangi.

Kamanda aliwataja watu hao kuwa ni Raymond Abasai(25) mkazi wa Tanga, Damiani Michaeli(30) mkazi wa Korogwe pamoja na Hasani Ramadhani (35) mkazi wa Mtongani jijini Dar es salaam.

Boaz aliongeza kuwa kilo 150 za bangi zilikamatwa katika Kijiji cha Makuyuni mji mdogo wa Himo julai 16 mwaka huu majira ya saa 2:00 mchana  mpakania mwa nchi jiranmi ya Kenya ikiwa imepakiwa kwenye pikipiki aina ya Honda yanye namba za usajili T161 CLG ikiwa inapelekwa Kenya.

Kamanda alisema mara baada ya kukamatwa dereva wa pikipiki hiyo alitelekeza pikipiki pamoja na bangi hiyo na kukimbilia kusikojulikana na kwamba anatafuta na polisi.

No comments:

Post a Comment