Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, July 18, 2014

NHIF YAIKOPESHA HOSPTALI YA KCMC ILI KUIWEZESHA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

MOSHI hosipitali ya rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro imetumia kiasi cha shilingi bilioni tatu (3,000,000,000) kwa ajili ya ujenzi wa majengo mawili ya wodi za wagonjwa wa uti wa mgongo na wagonjwa wa ngozi na hivyo kuondokana na adha ya kuwasafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi  kwa ajili ya matibabu ya maradhi hayo.

Mbali na ujenzi wa wodi hizo pia uongozi wa hospitali ya KCMC umeanza ujenzi wa jengo jipya la huduma za wagonjwa wa nje (OPD) kutokana na jengo la awali kuzidiwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya michoro ya jengo jipya la wagonjwa wa nje Kaimu mkurugenzi wa hospitali hiyo Profesa Raimos Olomi alisema jengo la zamani limejengwa zaidi ya miaka 40 iliyopita na kwa sasa halitoshelezi kutokana na wingi wa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.

Profesa  Olomi alisema jengo hilo litagharimu kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni mia tisa za kitanzania (1,900,000,000) fedha ambazo ni mkopo kutoka mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) na kusema kukamilika kwa majengo hayo kutaisaidia sana hospitali hiyo ambayo kwa sasa imezidiwa na ongezeko la wagonjwa huku eneo likiwa dogo.

Profesa  Olomi aliendelea kusema hospitali inauwezo wa kulaza wagonjwa 450 lakini kwa sasa wanalaza wagonjwa 520 -600.

Akikabidhi mchoro wa jengo hilo kwa mkandarasi  Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Dk. Martin Shao aliyaomba mashirika na watu binafsi kuunga mnkono juhudi za kanisa  kwa kuchangia ujenzi ili waweze kuboresha huduma na \kuifanya KCMC kuwa hospitali ya kimataifa ili kuwaondolea wagonjwa gharama za kutibiwa nje ya nchi.

Akizungumza katika hafla hiyo meneja wa NHIF mkoa wa Kilimanjaro Fidels Shauritanga alisema mkopo huo umetolewa na mfuko huo ili kuziwezesha hospitali kuwahudumia wateja wao kwa viwango vinavyotakiwa.

Alisema huo ni mkakati wa bodi ya wakurugenzi wa NHIF baada  ya kugundua hospitali nyingi haziwezi kutoa huduma bora kutokana na ubovu wa miundombinu na ukosefu wa vifaa tiba na ndio maana wamekubali kuzikopesha hospitali nyingi ili ziweze kutoa huduma nzuri kwa mgonjwa.

No comments:

Post a Comment