Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Friday, July 18, 2014

MTOTO AUAWA KIKATILI NA MUUAJI AJIKATA UUME WAKE NA KUULA KAMA KITOWEO

KILIMANJARO mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Francis Fortunatus  mwenye umri wa miaka (9) ameuwawa kikatili kwa kukatwakatwa na mapanga kichwani huku mtuhumiwa aliyetenda kosa hilo akijikata uume wake na kisha kufariki dunia. Tukio hilo la kusikitisha limetokea  wilaya ya Moshi vijijini Mkoani Kilimanjaro.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Robert Boaz, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 1:00 asubuhi julai 18 mwaka huu katika eneo la marangu kata ya marangu mashariki, jimbo la Vunjo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akielezea mazingira ya tukio hilo la kusikitisha kamanda Boaz, alisema kuwa mtoto huyo akiwa njiani akielekea shuleni gafla alivamiwa na mtu aliyejulikana kwa jina la Laurance Flavian (20) na kuanza kumkatakata kwa mapanga kichwa bila sababu yeyote na kusababisha kifo cha mtoto huyo papohapo.

Boaz alisema mara baada ya mtuhumiwa huyo kuona kuwa amesababisha mauaji alichukua panga alilo tumia kumkatakata mtoto huyo na kuamua kujikata uume wake mwenyewe.

Aidha alisema mara baada ya kijana huyo kujikata sehemu zake za siri alikimbizwa katika hosptali ya Kilema kwaajili ya matibabu na kwamba mara baada ya kufishwa hosptalini hapo alipoteza maisha kutokana na kuvuja damu nyingi.

Alisema chanzo cha tukio hilo kinaonyesha kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na ugonjwa wa akili na kwamba kabla ya kutenda tukio hilo alikuwa akifanya vurugu na kuvunja vunja vioo vya nyumba yao.

Hata hivyo habari za kuaminika kutoka katika eneo la tukio zinasema mara baada ya kijana huyo kumuua mtoto huyo aliula ubongo wake na  kukata uume wake na kula mwenyewe kama kitoweo.


Hivi karibuni katika eneo hilo kuliripotiwa matukio tofauti tofauti  ya kikatili kwa watoto ikiwemo kubwa la kulatiwa ni jambo lililozuwa hofu kubwa kwa wakazi wanao ishi maeneo hayo na maeneo ya jirani.

No comments:

Post a Comment