Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 10, 2014

WANAFUNZI NA SHULE ZITAKAZOFANYA VIZURI MITIHANI YA TAIFA KUPEWA ZAWADI

MWANGA Katika kuboresha na kuinua kiwango cha elimu na ufaulu kwenye kata ya lembeni, wilaya ya mwanga mkoani Kilimanjaro, kikao cha maendeleo cha kata WDC, kimeazimia kutoa zawadi  kwa wanafunzi na shule zitakazofanya vizuri katika mtihani wa taifa.

Hayo yameelezwa katika kikao
cha kata WDC, baada ya kikao hicho kuazimia kutoa motisha ya zawadi kwa mwanafunzi wa kwanza hadi watatu atakayefanya vizuri katika matokeo ya taifa ya darasa la saba.

Mratibu wa elimu kata ya lembeni, Sabasi Mayange, alisema mwanafuzi wa kwanza atazawadiwa laki moja na wa  pili atapewa elfu sabini na tano wakati mwafunzi wa tatu kwa ufaulu mzuri kwenye kata akijizolea kiasi cha shilingi elfu hamsini, Aidha shule ya kwanza kwa kufaulisha  vizuri itapewa kompyuta huku ya pili na ile ya tatu zikipewa radio kubwa.

Utekelezaji huo utaanza rasmi kwa matokeo ya wanafunzi wa darasa la saba  watakaofanya  mitihani yao ya taifa mwaka huu wa 2014.

No comments:

Post a Comment