Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 10, 2014

KITUO CHA AFYA KISANGARA CHATANGAZA KUWA NA DAWA ZA KUTOSHWA KWA WAGONJWA

MWANGA Imeelezwa kwamba kituo cha afya kisangara kilichopo kata ya lembeni, wilaya ya Mwanga katika mkoa wa Kilimanjaro, kina dawa za kutosha kutokana na uchangiaji wa bima ya afya kwa wananchi wanaotibiwa hospitalini hapo.

Hivyo wananchi wameshauriwa kuchangia bima ya afya ya mwaka kwa kila anayestahili kuchangia ili suala la upatikanaji wa dawa katika kituo hicho cha afya  liwe endelevu.

Mganga Mkuu wa kituo cha afya kisangara Dkt. Mashika E.
Mashika, akizungumza katika kikao cha WDC kata ya lembeni, alisema hakuna tatizo la dawa katika kituo cha afya kisangara na kwa sasa dawa zinapatikana kwa wingi  huku akiwasisitiza wananchi kuendelea kuchangia bima ya afya ili kuboresha zaidi huduma  za afya katika kituo chao.

Dkt. Mashika amesema mtu atakaye changia bima ya afya ya sh.10,000/= hatadaiwa gharama za matibabu kwa muda wa mwaka mmoja, ambapo pia bima hiyo itamwezesha mgonjwa aliyezidiwa kupelekwa hospitali ya wilaya usangi, mawenzi na KCMC kwa gari la wagonjwa bila kudaiwa gharama zozote.

Mwenyekiti wa kikao hicho cha kujadili maendeleo ya kata ya
lembeni,Namboleo Teri,amewasisitiza viongozi wa vijiji na watendaji wa kata hiyo kuwahimiza wananchi kuchangia bima ya afya katika kituo cha afya kisangara,ili upatikanaji wa dawa na huduma nyimgine za kiafya ziendelee kuwepo.

Mamboleo amesema kituo cha afya kisangara kinahudumia vijiji vingi vya kata  na  tarafa ya lembeni na endapo kila anayestahili kuchangia ada ya mwaka ya bima ya afya kiasi cha sh.10,000/= akifanya hivyo hapatakuwepo na malalmiko yeyote ya ukosefu wa dawa.

No comments:

Post a Comment