Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, July 10, 2014

Bank ya KCB Yatoa Msaada wa Mashine ya "ULTRA SOUND" kwa Hospitali ya MAWENZI

WAKAZI wa mkoa wa Kilimanjaro,  hususani wagonjwa, wameondokana na adha ambayo walikuwa wakiipata wakati walipokuwa wakifika katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa kilimanjaro  Mawenzi  kwa ajili ya matibabu, baada ya Hospitali hiyo kupatiwa  msaada wa mashine  ya (Ultra sound).

Wakizungumza wananchi hao, Mariam Mauld na Michael Mauki wamesema, wagonjwa wengi ambao walikuwa wakifika katika hospitali hiyo walishindwa kufanyiwa uchunguzi kutokana na mashine hiyo kutokuwepo.

Mauki ambaye ni mkazi wa kata ya Rau alisema, aliwahi kufika katika hospitali hiyo kwa lengo la kupima magonjwa ya Figo, lakini alishindwa kuhudumiwa kutokana na kutokuwepo kwa kipimo hicho, na kwamba kuwepo kwa mashine hiyo itasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wengi wakiwemo wa mama wajawazito.

 Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Mganga mfawithi wa hospitali ya Mawenzi, Dkt.  Lwezaura  Fredrick, alisema kwa takribani mwaka mmoja na nusu  hospitali hiyo ilikuwa haina kifaa hicho hivyo wagonjwa walikuwa wakilazimika kwenda katika hospitali za binafsi na ya rufaa KCMC kwa ajili ya uchunguzi.

Alisema "akina Mama  wajawazito ambao walikuwa wakifika hapa kwa ajili ya kupima walikuwa wakipata changamoto kubwa ya ukosefu wa kifaa hicho, na kwamba tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi baada ya    benki ya KCB ya mjini Moshi, kutoa msaada huo wenye  thamani ya Shilingi milioni  15. lengo likiwa ni kutatua adha waliyukuwa wakiipata wagonjwa hao."Amesema wagonjwa wengi walikuwa wakilazimika kwenda katika hospitali binafsi na kutibiwa kwa garama kubwa, na kwamba kuwepo kwa kuwepo kwa mashine hiyo katika hospitali hii itatatua changamoto  hizo.

Awali akikabithi mashine ya ultra saund meneja wa benki ya KCB Moshi, Oforo Erasmo, amewaomba kuitumia  mashine hiyo vizuri na kuitunza ili idumu pamoja na kuwasaidia wagonjwa wengi wa mjini Moshi.

Erasmo  alisema kwa mwaka huu KCB imetenga jumla ya Shilingi milioni 350,  kwa ajili ya kuhudumia jamii nchi nzima, katika nyanja za kielimu, Afya, Maji na Mazingira.

Naye  kaimu katibu tawala mkoa wa kilimanjaro Mhandisi, Alfred Shayo, amepongeza benki ya KCB kwa msaada waliotoa hali ambayo itasaidia kuboresha afya za wagonjwa.

No comments:

Post a Comment