HAI
baraza la Madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Hai, Mkoani
Kilimanjaro limemchagua Ally Mwanga ambae ni Diwani wa kata ya
Masama Mashariki (CCM) kuwa makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
kwa kipindi cha kuanzia Julai 2014 hadi June 2015.
Mwanga alichaguliwa kwa kupigiwa kura za siri za ndio au hapana baada
ya mgombea wa Chama cha Demokransia na Maendeleo (CHADEMA) kujitoa
kutokana na maridhiano walikubaliana wajumbe wa baraza hilo linaloundwa
na vyama viwili vya Siasa vya CCM na CHADEMA.
Uchaguzi huo wa kumchagua makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
ulifanyika katika ukumbi wa Halamashauri ambapo vyama hivyo viwili
vilikubaliana nafasi ya makamu mwenyekiti iendelee kushikiliwa na diwani
wa CCM kutokana na kuongozwa na Mwenyekiti anayetoka CHADEMA.
Awali akitangaza matokeo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo
Melekzedeck Humbe alisema Mwanga alipata kura 18 kati ya 19 zilizopigwa
huku moja ikiharibika.
Baraza hilo la madiwani pia liliwachagua wajumbe na wenyeviti
mbalimbali wa kamati watakao ongoza kwa pindi cha mwaka mmoja
cha kuanzia Agosti 2014 hadi June 2015.
No comments:
Post a Comment