Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, August 6, 2014

IDADI YA VIFO KWA WAJAMZITO NA WATOTO VYAPATIWA SULUHISHO LA KUDUMU

MOSHI ongezeko kubwa la wanawake wajawazito wanaohudhuria kituo cha afya kata ya Pasua katika manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, imeongezeka kutoka wanawake 528 mwaka 2010, hadi kufikia wanawake 726 mwaka 2013.


Ongezeko hilo ambalo linasaidia kupunguza idadi ya kubwa ya vifo vya wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kutokana na wanawake kuhamasishwa kuhudhuria kliniki mara baada ya kubaini kuwa ni mjamzito.


Kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Moshi Dk. Boaz Mwaikugile alisema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari wa mtandao huu, chini ya mpango wa Uhai wa akina mama na watoto wachanga.


Alisema Vifo vya kina mama wajawazito Manispaa ya Moshi ni  254 kati ya 100,000 na watoto chini ya miaka mitano  ni vifo 19 kati ya 1,000 kwa kipindi cha 2012/2013.


Aidha Dk. Mwaikugile alisema Vifo vingi katika Manispaa ya Moshi vinatokea Hospitali ya rufaa ya kanda KCMC ambapo vinachangiwa na wagonjwa wanaocheleweshwa kufika katika hospitali hiyo kwani baadhi wanatokea wilayani, mikoa mbalimbali nchini  na wengine nchi za jirani kama Kenya.


“Kampeni tunazofanya kwa sasa hivi ni kuhamasisha wanawake mara wanapobaini kwamba ni wajawazito wahudhurie kiliniki kwa miezi yote hadi watakapojifungu. hii itasaidia kuepusha vifo visivyo vya lazima” alisema Dk. Mwaikugile.


Dk. Mwaikugile alisema kituo cha afya kata ya Pasua kwa mwezi kinahudumia wastani ya wagonjwa wa nje 925, mama wajawazito 125 wanahuzuria kliniki, wajawazito 65 wanajifungua na watoto chini ya miaka mitano 146 wanaudhuria kliniki.



Kwa upande wao baadhi ya wanawake wanaohudhuria kliniki katika kituo hicho, Mwamvita Ally, Agness Mushi  na Asia Hemed walidai utoaji wa huduma katika kituo hicho umeboreshwa ambapo hapo awali iliwalazimu wanawake kwenda na vifaa vya kujifungulia lakini sasa vifaa hivyo vinapatikana katika kituo hicho.


“Unapohudhuria unapewa tahadhari kwamba ununue vifaa vya kujifungua kama mipira ya mikononi, dawa na sindano kwa ajili ya kuzua damu, hii ni kwa vile wengi wetu tunaishi mbali na kituo cha afya, ikitokea dharura uweze kusaidiwa kabla ya kufika kituo cha afya” alisema Ally.

No comments:

Post a Comment