KILIMANJARO serikali mkoani Kilimanjaro imewataka wananchi kujiwekea
akiba ya chakula katika kipindi hichi cha mavuno na kuacha kutumia nafaka kwa
kutengenezea pombe za kienyeji, lengo likiwa ni kukabiliana na kipindi cha njaa.
Mkuu wa mkoa wa kilimnjaro Leonidas Gama, aliyasema hayo
wakati akizungumza na mmoja muandishi wa mtandao huu jana
Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro ambapo alisema hali ya kilimo na upatikanaji wa
chakula ni ya kuridhasha.
Alisema mkoa wa Kilimanjaro baadhi ya wilaya zake zimekuwa zikikabiliwa na
njaa kutokana na wananchi kutokuwa na
desturi ya kujiwekea akiba ya chakula katika kipindi cha mavuno na kutumia
nafaka katika utengenzaji wa pombe za kienyeji.
Alisema mkoa
ulijiwekea malengo ya kuvuna na kukusanya zaidi ya tani Milioni 1.9 katika
kipindi cha mwaka 2013/2014 na kwamba
hali ya upatikaji wa chakula ni ya kuridhisha ambapo katika
kipindi cha mwaka 2014 wanatarajia kuvuna kuvuka lengo hilo.
Aidha aliziagiza halmashauri za wilaya kupitia wataalamu wa kilimo mkoani Kilimanjaro
kuwaelimisha wananchi juu ya njia bora za kuhifadhi mazao ili kusaidia vyakula hivyo kuto haribika
kwa haraka.
No comments:
Post a Comment