Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Thursday, August 7, 2014

MKOA WA KILIMANJARO UMEFANIKIWA KUJENGA MAABARA ZAIDI YA 130

KILIMANJARO maabara zaidi ya 130 zimejengwa katika mkoa wa Kilimanjaro kwenye shule mbalimbali za sekondari, kwa lengo la kuboresha masomo ya sayansi katika shule hizo na mkoa huo kwa ujumla.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na agizo la Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, lililowataka viongozi wa mikoa yote Tanzania kuhakikisha kila shule ya sekondari inakuwa na maabara.

Mkuu huyo wa mkoa wa Kilimanjaro alisema katika kutekeleza mpango huo kumekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya wananchi kuwa na ugumu wa kutokuwa na ushirikiano katika ujenzi wa maabara hizo ili kufanikisha zoezi hilo.

Aidha Gama aliwataka wananchi kuona umuhimu wa kuchangia miradi ya maendeleo katika maeneo yao ikiwemo sekta ya elimu na kwamba mbali na juhudi za serikali michango inayotolewa na wananchi ni muhimu kwa ajili ya maendeleo.

Alisisitiza na kutoa wito kwa wanafunzi kuhakikisha wanajituma katika elimu ili kuenzi juhudi zinazofanywa na serikali pamoja na wananchi katika kuchangia miradi ya elimu.

No comments:

Post a Comment