Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 24, 2014

Chuo Kikuu Kishiriki "MUCCOBS" chapanda hadhi na kuwa chuo kikuu kamili "Moshi Cooperative University"



KILIMANJARO tume ya vyuo vikuu nchini, (TCU), imekipandisha hadhi chuo kikuu kishiriki cha ushirika na biashara mkoani Kilimanjaro MUCCoBS kuwa chuo kikuu kamili kitakachojulikana kama chuo kikuu cha ushirika Moshi, (MoCU).

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo Philemon L. Luhanjo, wakati wa hafla ya kutangaza mabadiliko ya chuo kikuu kishiriki cha ushrika Moshi, (MUCCoBS).

Aidha Luhanjo alitangaza mabadiliko makubwa katika chuo kikuu hicho kipya kuanzia Julai 3, mwaka huu ambapo alisema ni pamoja na jina la chuo hicho kuwa chuo kikuu cha ushirika Moshi, (MoCU).

Aidha alisema kuwa katika uteuzi huo Prof. Gerald Monele ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la mpito la MoCU, ambapo Prof. Faustine Bee, ameteuliwa kuwa   kaimu makamu mkuu wa chuo kikuu hicho kipya.

Akizungumza katika hafla hiyo, mwenyekiti wa baraza la mpito la chuo kikuu cha ushirika Moshi, (MoCU), Prof. Gerald Monela, aliahidi kushirikiana na wadau mbalimbali katika kukamilisha yale yaliyo ambayo serikali inategemea yafanyike.

No comments:

Post a Comment