Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 24, 2014

Muwezeshaji kutoka bank ya KCBL awahasa watanzania kuwa mikopo huinua na kuboresha maisha

KILIMANJARO chama cha Akiba na Mikopo cha wakulima wa mpunga (CHAMIWAMKA), cha eneo la Kaloleni, manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kimeazimia kutafuta masoko ya nje ya mazao yao.
 
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa chama hicho Bw. Maulid Athuman, wakati wa semina ya mafunzo kwa wanachama wa chama hicho pamoja wakulima wa mpunga ambao si wanachama wake, iliyofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, hivi karibuni.
 
“Ili kutimiza azma yetu, uongozi wa chama chetu umeanza mikakati ya kuomba leseni kwa ajili kuuza nje ya nchi mpunga tunaozalisha ili kukiongezea chama chetu na wanachama wetu mapato”, alisema Bw. Maulid Athuman,.
 
Aidha Bw. Abdhalla alisema chama hicho pia kimeanza mikakati ya kuanzisha miradi mingine ambayo itasaidia kukiongezea chama hicho mapato pamoja na wakulima ambao ni wanachama wa chama hicho.
 
Akiongea katika semina hiyo, mwezeshaji wa semina hiyo Bw. Ahsanterabi Msigomba kutoka benki ya ushirika mkoani Kilimanjaro, KCBL, alisema kuwa chama hicho tayari kinafanya kazi na vyama vya ushirika 238, vikiwemo vile vya akiba na mikopo, (Saccos), vyama vya kilimo na masoko, (Amcos), pamoja na vyama vikuu vya ushirika mkoani Kilimanjaro, vya KNCU  na Vuasu.
 
“Ushirikiano wetu wa kibiashara na vyama hivi umekuwa wa mafanikio makubwa hivyo nitoe rai kwa wale wakulima ambao hawajajiunga na CHAMIWAMKA kufanya hivyo ili waweze kufaidi ushirikiano huu”, alisema Bw. Msigomba.
 
Aidha alitoa rai kwa wakulima na wafanyabiashara kuepuka dhana potofu kuwa mikopo huwa inafilisi ambapo alisema mikopo huinua na kuboresha maisha ya wale wote wenye kuitumia kama ilivyo kusudiwa.

No comments:

Post a Comment