Banner

Banner

FOLLOW US FACEBOOK

propertyfinder.co.tz

Wednesday, September 24, 2014

Serikali imeanza kusambaza mbegu za mtama bure kwa wakulima ili kukabiliana na janga la njaa

KILIMANJARO serikali imeanza   kusambaza mbegu bora  za kisasa za mtama kwa wakulima wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro, lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi kukabiliana na janga la njaa katika kipindi cha ukame ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kiuchumi.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi Dkt. Ibrahim Msengi,  wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mjini Moshi mkoani hapa ambapo alisema katika kukabiliana na janga la njaa kwa wananchi serikali imeanza  kutoa mbegu hizo bure kwa wakulima.

Dkt. Msengi  alisema wilaya hiyo katika maeneo yake ya tambarare kila mwaka yamekuwa yakikabiliwa na janga la njaa na kulazimika kupata chakula cha msaada kutoka serikalini kwa aajili ya kunusuru hali hiyo na kwamba kutokana na suala hilo wilaya hiyo imeanza mchakato wa kusambaza mbegu  bora za zao la mtama ambalo huvumilia ukame.

Aidha alisema kumekuwa na mashamba darasa ya kilimo cha zao hilo kwaajili ya kuhamasisha wananchi na wakulima kujihusisha na kilimo cha zao hilo ambapo kwasasa  watu wengi  wamehamasika na  wamejitokeza na kutaka kuanza kulima mtama.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kujitokeza na kujihusiha na kilimo cha zao la mtama kwaajili ya chakula na biashara ili kuweza kujikwamua katika wimbi la umasikini.

Katika hatua nyingine Dkt. Msengi aliwataka wananchi kuhifadhi na kutunza chakula walicho nacho katika msimu huu wa mavuno kwaajili ya kukabiliana na janga la njaa.

No comments:

Post a Comment